Kikao cha Bawacha chasambaratishwa, Halima Mdee, wabunge mbaroni

Kikao cha Bawacha chasambaratishwa, Halima Mdee, wabunge mbaroni

13 July 2019 Saturday 14:52
Kikao cha Bawacha chasambaratishwa, Halima Mdee, wabunge mbaroni

Na mwandishi wetu, Bariadi
JESHI la polisi wilayani  Bariadi mkoani Simiyu wamevamia na kupiga mabomu kusambaratisha kikao cha ndani cha Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) kilichokuwa kinaongozwa na mwenyekiti wa taifa, Halima Mdee akiwa na katibu mkuu, Grace Tendega  na wabunge wengine.


Taarifa ya Chadema inaeleza kuwa leo Julai 13, 2019 Polisi wakiwa na silaha za moto wakiwa katika magari wakiongozwa na OCA na OCCID wamevamia kikao hicho kilichokuwa kinafanyika katika ukumbi wa Double S mjini Bariadi na kumlazimisha mmiliki kufungua mlango wa dharura baada ya kushindwa kupita milango ya mbele iliyokuwa imefungwa.


"Baada kuingia ndani wamelazimisha wanachama kutoka nje na kuwataka kuondoka eneo hilo wakidai kuwa kikao si halali, kisha wakaanza kupiga mabomu ya machozi, kukamata viongozi na wanachama" inaeleza taarifa hiyo 

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.