Lissu kushiriki uchaguzi serikali za mitaa 2019

"Kurejea kwake nyumbani kunakamilisha miaka miwili ya matibabu yake nje ya nchi baada ya kupigwa risasi mjini Dodoma, Septemba 7, 2017"

Lissu kushiriki uchaguzi serikali za mitaa 2019

"Kurejea kwake nyumbani kunakamilisha miaka miwili ya matibabu yake nje ya nchi baada ya kupigwa risasi mjini Dodoma, Septemba 7, 2017"

22 May 2019 Wednesday 10:27
Lissu kushiriki uchaguzi serikali za mitaa 2019

 
Na mwandishi wetu, Singida
HATIMAYE mbunge Tundu Lissu (Chadema) anatarajiwa kutua nchini mwezi Septemba, 2019 na atashiri katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwishoni mwaka  2019.

Pia anatarajiwa kupokelewa na viongozi, wafuasi na wanachama mbalimbali.

Lissu amethibitisha  hilo  kwa njia ya simu mubashara katika mkutano wa ndani wa Chadema uliofanyika jana jioni mkoani Singida katika wilaya ya Ikumbi.


Akiongea katika mkutano huo uliokuwa ukiongozwa na mwenyekiti taifa wa Chadema, Freeman Mbowe, Lissu amesema Septemba 7, 2019 atawasili nchini.

Amesema pamoja na mambo mengine atashiriki kufanya kampeni katika uchaguzi wa serikali za mitaa. Uchaguzi huo unatarajiwa  kufanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba, 2019

Baada ya kupokewa  Tundu Lissu   atazungumza na Watanzania kupitia vyomba mbalimbali vya habari.


Kurejea kwake nyumbani kunakamilisha miaka miwili ya matibabu yake nje ya nchi baada ya kupigwa risasi mjini Dodoma, Septemba 7, 2017.

Tundu Lissu ni mbunge wa Singida Mashariki, na pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema.

Aliwahi kuwa rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).
Updated: 22.05.2019 13:24
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.