Maalim Seif Sharrif Hamad mbioni kuondoka CUF?

Atoa kauli tata kuhusiana na mwaliko kwenda CHADEMA

Maalim Seif Sharrif Hamad mbioni kuondoka CUF?

Atoa kauli tata kuhusiana na mwaliko kwenda CHADEMA

14 September 2018 Friday 12:15
Maalim Seif Sharrif Hamad mbioni kuondoka CUF?

TAMKO la Maalim Seif Shariff Hamad, Katibu Mkuu wa CUF kwamba ‘muda ukifika nitazungumza’ kuhusu kuhama chama hicho inatikisa msimamo wake wa awali.

Tamko hilo amelitoa ikiwa ni siku nne baada ya kupata ‘mwaliko’ wa kujiunga na Chadema ambapo ameahidiwa kugombea nafasi ya urais visiwani Zanzibar kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.

Ahadi hiyo ya Chadema ilitolewa na Hashim Juma, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Chadema.

Maalim Seif amesema kwamba, kwa sasa hawezi kuzungumzia suala la kwenda Chadema kwa sasa na kwamba, wakati ukifika atazungumza na waandishi.

Kauli ya Maalim Seif iliwasilishwa na Nassor Ahmad Mazrui, Naibu Katibu Mkuu wa CUF-Zanzibar

Kauli hiyo ya Maalim Seif inaonesha kulegeza msimamo wake wa awali kwamba hawezi kuhama CUF.

Msimamo huo unafanana na ule wa Ally Saleh, Mbunge wa Malindi (CUF) kwamba, wakati ukigika watajua wafanye nini ili wabaki kwenye Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Tayari Magdalena Sakaya, Naibu Katibu Mkuu CUF Bara amemtahadharisha Maalim Seif kwamba, akihama CUF itakuwa ndio mwisho wake wa siasa.

Updated: 14.09.2018 12:24
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.