Magufuli aahidi maendeleo bila ubaguzi wa kisiasa

Magufuli aahidi maendeleo bila ubaguzi wa kisiasa

04 September 2018 Tuesday 18:42
Magufuli aahidi maendeleo bila ubaguzi wa kisiasa

Rais John Magufuli ameahidi kutumia ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutekeleza miradi ya maendeleo hata kwenye majimbo na kata zilizochagua wabunge na madiwani kutoka vyama vya upinzani.

Akihutubia mkutano wa hadhara mjini Nansio, Makao Makuu ya wilaya ya Ukerewe leo Septemba 4, 2018 Rais Magufuli amesema anafanya hivyo kwa sababu maendeleo hayana itikadi ya vyama huku akiwashukuru wakazi wa wilaya hiyo kwa kumchagua licha ya yeye kutofika kuwaomba kura mwaka 2015.

"Ukerewe mlinipigia kura ni lazima muonje maendeleo yanayoletwa na CCM ambayo ndiyo ilani yake inatekelezwa," amesema.

Ametumia fursa hiyo kummwagia sifa mbunge wa Ukerewe, Joseph Kakunda (Chadema) kwa kuishukuru Serikali kwa kutekeleza miradi ya maendeleo wilayani humo akimtania kuwa sura yake inaonyesha yuko upinzani lakini moyo wake unaonyesha yuko CCM, kauli iliyopokelewa kwa shangwe na wananchi.

Akisisitiza umuhimu wa ilani ya CCM kutekelezwa kote nchini, Rais amesema viongozi wote kuanzia mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wa halmashauri wote wanatokana na chama hicho tawala lakini bado wanapeleka na kutekeleza miradi ya maendeleo hata kwenye maeneo ambayo wananchi walichagua wawakilishi kutoka vyama vya upinzani.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.