Mbunge Bwege aendelea kusota rumande

"Mbunge huyo alikamatwa mara baada ya kumaliza kusikiliza kesi nyingine inayomkabili mkoani Lindi ya kutaka kufanya mkutano wa hadhara bila kuwa na kibali"

Mbunge Bwege aendelea kusota rumande

"Mbunge huyo alikamatwa mara baada ya kumaliza kusikiliza kesi nyingine inayomkabili mkoani Lindi ya kutaka kufanya mkutano wa hadhara bila kuwa na kibali"

25 May 2019 Saturday 11:19
Mbunge Bwege aendelea kusota rumande

Na mwandishi wetu, Kilwa
MBUNGE wa Kilwa Kusini mkoani Lindi, Suleiman Bungara maarufu Bwege(CUF), ameendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo baada ya kunyimwa dhamana hapo jana Mei 24, 2019


Mbunge huyo  alikamatwa jana  mara baada ya kumaliza kusikiliza kesi nyingine  inayomkabili mkoani Lindi ya kutaka kufanya mkutano wa hadhara bila kuwa na kibali.

Bwege anashikiliwa akidaiwa kwa tuhuma za uchochezi kufuatia mkutano wake na wavuvi mjini Kilwa Kivinje Mei 23, 2019.

Katika mkutano huo inadaiwa Bwege amewataka wavuvi kukata leseni za uvuvi na si kulipia kitambulisho cha ujasiliamali kama walivyoamriwa na mkuu wa mkoa.

Kwa mujibu wa chanzo chetu ndani ya Jeshi la Polisi  kimesema uenda mbunge huyo akaachiliwa kwa dhamana Jumatatu ya  Mei 27, 2019


Bwege yupo mahabusu katika  kituo kikuu cha cha polisi Lindi na inadaiwa Jeshi la Polisi linakataa kutoa dhamana kwa hoja kuwa wao wamepokea amri ya kumkamata hivyo wanasubiri maelekezo.

Kukamatwa  huko ni muendelezo kwa mbunge huyo machachari, Oktoba 2, 2018  alikamatwa na polisi akidaiwa kutaka kufanya mkutano wa hadhara bila kuwa na kibali.

Updated: 25.05.2019 11:31
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.