Mbunge wa CUF Seleman Bungara 'Bwege' ashikiliwa na polisi

Mbunge wa CUF Seleman Bungara 'Bwege' ashikiliwa na polisi

01 October 2018 Monday 22:42
Mbunge wa CUF Seleman Bungara 'Bwege' ashikiliwa na polisi

Mbunge wa Kilwa Kusini (CUF), Seleman Bungara 'Bwege' anashikiliwa na polisi akidaiwa kutaka kufanya mkutano wa hadhara bila kuwa na kibali.

Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai akizungumza kupitia mtandao wa gazeti la kila siku la Mwananchi jioni hii, amesema Bwege amekamatwa saa 10 jioni eneo la Maalim Seif  lililopo Kilwa Kivinje.

Ngubiagi amesema mbali na Bwege wengine wanaoshikiliwa na polisi ni madiwani wanne akiwemo diwani wa Kilwa Masoko na mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Abuu Mjaka.

"Bungara alipeleka barua ila kwa sababu za kiusalama polisi walizuia mkutano huo na yeye aliomba asiufanye. Endapo angefanya kungekuwa na uvunjifu wa amani," amesema Ngubiagai ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.