Mdude: Nilitekwa na watu tisa

"Tukio hili ni la kisiasa lilipangwa kwa lengo la kuniua".

Mdude: Nilitekwa na watu tisa

"Tukio hili ni la kisiasa lilipangwa kwa lengo la kuniua".

20 May 2019 Monday 13:54
Mdude: Nilitekwa na watu tisa

Na mwandishi wetu, Dar es salaam
KADA wa Chadema, Mdude Nyagali amesema  alitekwa na watu tisa, kuteswa  hadi kupoteza fahamu.

Amesema tukio lake hilo ni la kisiasa na  lilipangwa kwa lengo la kumuuwa na kwamba hatua yake ya kuikosoa serikali na rais Magufuli ndio sababu kubwa ya kukamatwa kwake.

Amesema hayo leo Mei 20, 2019 jijini Dar es salaam katika mkutano wake na waandishi wa habari.

"Nilitekwa na watu tisa, walinipiga hadi nikapoteza fahamu. Msingi wa tukio langu ni siasa," amesema

Akisimulia jinsi alivyotekwa amesema watekaji hao walifika ofisini kwake eneo la  Vua Mbozi majira ya saa kumi na moja jioni ya Mei 4, 2019 siku ya Jumamosi, wakiwa na gari mbili aina ya Land Cruser had top nyeupe na Nissan Patrol ambayo mojawapo haikuwa na namba ya gari.

" Mara tu nilipotoka ofisini watu watatu walishuka katika ile Land Cruiser wakanifuata na kunizunguka na kuanza kunihoji, mara  wakaninyanganya simu na begi lililokuwa na lap top HP na nyaraka mbalimbali za chama na zangu binafsi," amesema

Amesema baada ya kudhibitiwa watu hao, alipiga kelele kuomba msaada na ndipo watu wawili waliongezeka kutoka katika gari aina ya  Nissan Patrol na kuendelea kumdhibiti  na mmoja wao alimuonyesha bastola.

"Walinidhibiti kwa kuniziba mdoma huku wakinipiga kichwani na kwa mbele nilimuona mtu mwingine akiwa ameshika bastola akiwatishia watu wasije kunipa msaada, na walifanikiwa kuniingiza kwenye buti la ile LandCruiser na mmoja alinikanyaga tumboni na wengine waliendelea kunipiga kichwani na gari likaondoka kuelekea njia ya barabara kuu iendayo Mbeya hadi Dar es Salaam kutokea mkoani Songwe,'' amesema Mdude

 

"Cha ajabu nilipotekewa kuna umbali wa mita 300 hadi 400 ilipo makao makuu ya Polisi, mita 50 yapo makazi ya askari Polisi,'' amesema

Amesema baada ya kipigo cha muda mrefu alianza kuvuja damu puani, mdomoni na sikioni na alipoteza fahamu na alipopata fahamu alijikuta polini akiwa kazibwa mdomo na macho.


"Sikuwa na nguvu kabisa, nilianza kutambaa na kutembea kidogo na kuanguka hadi nikafika barabarani kuomba msaada lakini magari yalinipita. Takribani saa moja ndipo alipotokea pikipiki ikasimama, lakini alishindwa kunibeba akaenda kumchukua mwenzake, wakanipeleka  Inyala,'' amesema

Ndipo mwenyekiti wa kijiji cha Inyala akatoa taarifa kwa viongozi wa chama na jeshi la polisi.

"Waliniokota nikiwa na suruali , koti na vitambulisho vitatu na nakumbuka nilikuwa na Tsh10000 lakini haikuwepo,'' amesema

Amesema alipigwa kichwani, mgogoni na kwamba hadi sasa anaendelea na matibabu

Hilo ni tukio la pili kwa kada huyo wa Chadema kutekwa, aliwahi kutekwa mwaka 2016.

Updated: 20.05.2019 22:18
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.