Mnangagwa kuingia kwenye mtihani wa Urais mwishoni mwa Julai

Mnangagwa kuingia kwenye mtihani wa Urais mwishoni mwa Julai

30 May 2018 Wednesday 18:15
Mnangagwa kuingia kwenye mtihani wa Urais mwishoni mwa Julai

Na Mwandishi Wetu

RAIS wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa anatarajia kuingia kwenye kinyanga’nyiro cha urais kwa mara ya kwanza mara baada ya kuondolewa kwa Robert Mugabe mwaka jana.

Tayari ametangaza kuwa Zimbabwe itafanya uchaguzi mkuu miezi miwili kuanzia sasa, yaani tarehe 30 mwezi Julai

Kiongozi huyo ametangaza hivyo kupitia waraka maalum wa serikali uliochapishwa hii leo.

Waraka huo umetangaza kuwa tarehe hiyo pia utafanyika uchaguzi wa wabunge na wa serikali za mitaa.

Rais Mnangagwa pia amesema duru ya pili ya uchaguzi wa rais itafanyika Septemba 8 mwaka huu, kama atakosekana mgombea atakayeshinda kwa asilimia 50 ya kura.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.