banner68

Mtatiro si mwanachama CUF, atakiwa akae mbali

Mtatiro si mwanachama CUF, atakiwa akae mbali

11 July 2018 Wednesday 13:57
Mtatiro si mwanachama CUF, atakiwa akae mbali

Jumuiya za Vijana za CUF (JuviCUF) wilaya za Dar es Salaam, zimemtaka Julius Mtatiro kukaa mbali na chama hicho na kuacha tabia ya kuwashambulia viongozi wa juu wa CUF kupitia mitandao ya kijamii kwa kuwa yeye sio mwanachama.

Kauli hiyo imetolewa leo, Jumatano Julai 11, 2018 na mwenyekiti wa JuviCUF wilaya ya Ilala, Canal Kitimai kwa niaba ya viongozi wenzake wa wilaya wakati akizungumza na wanahabari.

Kitimai amesema Mtatiro siyo mwanachama wa chama hicho lakini amekuwa tabia ya kuandika maandiko kwenye mitandao ya kijamii yanayolenga kuivuruga CUF.

“Aache hii tabia ya kuingilia masuala ya CUF. Kama Serikali itashindwa kumdhibiti, sisi kwa kutumia Katiba yetu tutamshughulikia kisha tutampeleka kwenye vyombo vya dola,"amesema Kitimai.

Kitimai amesema hivi karibu Mtatiro kupitia akaunti yake ya Facebook aliandika maandiko ya kuwashambulia viongozi chama hicho kuhusu hatua ya hatua ya kuvuliwa uanachama madiwani watatu wa CUF mkoani Tanga.

Juzi Mtatiro ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF upande wa Maalim Seif Sharif Hamad alimtuhumu Magdalena Sakaya kutumiwa na CCM ili kukivuruga chama hicho.

Hata hivyo, Sakaya alimjibu kuwa hana sababu ya kujibizana na Mtatiro kwa kuwa CUF inaongozwa na Katiba.

Lakini leo Kitimai amesema hawatambui Mtatiro ndani ya CUF na kama hana shughuli za kufanya aseme atafutiwe ili aache tabia ya kuwashambulia viongozi wa juu wa chama hicho.

Kitimai amesisitiza kuwa uamuzi wa kuwavua uanachama madiwani watatu kwa sababu ya utovu wa nidhamu ni sahihi na Mtatiro aache kupotoshwa umma kupitia maandiko yake.

Akizungumzia kauli hiyo, Mtatiro amesema, " Siwezi kuwajibu hao JuviCUF. Mtafute Maharagande (Mbarala- naibu  mkurugenzi wa habari na  mawasiliano upande wa Maalim Seif"

Alipotafutwa Maharagande naye alitoa maelekezo atafutwe Mwenyekiti wa JuviCUF Taifa, Hamidu Bobali  alizungumzie jambo hilo.

Bobali amesema tamko hilo lilitolewa na Kitimai ni batili kwa kuwa hana mamlaka ya kuzungumzia masuala hayo.

"Nimesikia wanasema mwenyekiti wa JuviCUF Taifa hajitambui yupoyupo tu, ndio maana wakaamua kuzungumzia.Sasa nawaambia Mimi nipo imara na walichokisema hakina baraka kutoka kwangu,"amesema Bobali ambaye pia Mbunge wa Mchinga.

Mwananchi

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.