Mvutano mkali watokea kuhusu mazishi ya Bilago, Chadema wasusia gari

Mvutano mkali watokea kuhusu mazishi ya Bilago, Chadema wasusia gari

29 May 2018 Tuesday 13:00
Mvutano mkali watokea kuhusu mazishi ya Bilago, Chadema wasusia gari

Mvutano mkubwa umetokea kuhusu mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Buyungu, kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA), Kasuku Bilago, huku kila upande ukipanga tarehe yake.

Katika ratiba iliyotolewa na Bunge imesema kuwa Bilago anatarajiwa kuzikwa kesho tarehe 30/ Mei 2018 mkoani Kigoma, lakini chama chake kimedai kuwa atazikwa keshokutwa.

Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Stephen Kagaigai amesema kuwa ratiba iliyotolewa na bunge ndiyo sahihi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kuwa mwili wa marehemu Bilago utazikwa keshokutwa mkoani Kigoma.

“Labda waulize Bunge wanazika kesho mwili wa nani, wamewasiliana na chama gani au familia gani, sisi tunazika keshokutwa na tutaondoka mara baada ya kuaga hapo bungeni,” amesema Mbowe

Hata hivyo, Wabunge wa Chadema wamegoma kupanda gari lililoandaliwa na bunge kuwapeleka Kigoma kwa ajili ya kuhudhuria mazishi, huku wakidai kuwa wamekodi basi lao, hivyo basi la bunge litabeba wabunge wa CCM.

Dar24

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.