Mwingine aikacha Chadema na kutimkia CCM

Mwingine aikacha Chadema na kutimkia CCM

28 September 2018 Friday 08:56
Mwingine aikacha Chadema na kutimkia CCM

MBUNGE wa Serengeti (Chadema), Marwa Chacha amejiuzulu uanachama wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

Akizungumza leo Septemba 27, 2018 Chacha amesema amechukua uamuzi huo kumuunga mkono mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli.

Amesema wakati akigombea ubunge aliahidi kuwaletea maendeleo wananchi wake lakini dhamira yake haijafanikiwa kutoka na vikwazo anavyokumbana navyo ndani ya Chadema.

Chacha amewataka wakazi wa Serengeti kumchagua mtu atakayeweza kushirikiana nao pamoja ili kuleta maendeleo kupitia CCM.

Mbunge huyo alikutana na wakati mgumu wakati wa ziara ya Rais Magufuli mkoani Mara ya kuzomewa na wananchi alipobanwa na maswali.

Baada ya kuzomewa Chacha alipopata nafasi kuzungumza alisema, wanamzomea kwa sababu yeye siye CCM lakini ipo siku naye atakuwa CCM.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.