Mwinyi amnadi Magufuli urais 2020

"Rais Magufuli ameiomba serikali ya Saudia Arabia kujenga chuo kikuu kipya cha waislam nchini"

Mwinyi amnadi Magufuli urais 2020

"Rais Magufuli ameiomba serikali ya Saudia Arabia kujenga chuo kikuu kipya cha waislam nchini"

19 May 2019 Sunday 14:44
Mwinyi amnadi Magufuli urais 2020

Na mwandishi wetu, Dar es salaam
RAIS mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi amewaomba watanzania kumchagua tena, rais Dkt. John Magufuli katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020.

Mwinyi ameyasema hayo  leo  Mei 19, 2019 jijini Dar es salaam, uwanja wa taifa katika mashindo ya 20 ya kuhifadhi Quran Afrika yaliyoandaliwa na taasisi ya Al-Hekma foundation ambapo rais Magufuli alikuwa mgeni rasmi.


Amesema ombi lake hilo ni ili aendeleze shughuli za maendeleo alizozianzisha.

"Ningependa, ningeomba katika awamu inayokuja rais Magufuli achaguliwe tena kuwa rais  ili uendeleze uliyoanzisha," amesema Mwinyi

Awali rais Magufuli alilisisitiza kudumishwa kwa umoja wa watanzania na kwamba ndio njia bora ya kudumisha amani.

Pia ameagiza taasisi ya Al-Hekma kupewa eneo la wazi lililopo karibu na taasisi hiyo  ili liendelezwe kwa kujengwa hospitali.

"Najua umuhimu wa eneo hilo, pia najua umuhimu wa taasisi hii hivyo naagiza  hadi kufikia Ijumaa ijayo eneo hilo likabidhiwe rasmi kwa taasisi ya Al Hakma na mjenge hiyo Hospitali, kumbukeni nitafuatilia,'' amesema rais Magufuli

 Aidha rais Magufuli ameomba kuongezwa idadi ya washiriki kutoka 19 hadi idadi ya nchi zote za Afrika.

Pia ameiomba serikali ya Saudia Arabia kujenga chuo kikuu kipya cha waislam nchini.

Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza wa juzuu 30 amekuwa ni Mohamad  Diano kutoka nchini Senegal na apewa zawadi ya milioni 20 za kitanzania na zawadi ya tiketi ya dege kwenda kufanya ibada ya  Hijja
Updated: 19.05.2019 14:58
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.