Mwita Waitara arudi tena Ukonga

Mwita Waitara arudi tena Ukonga

17 September 2018 Monday 12:23
Mwita Waitara arudi tena Ukonga

MGOMBEA Ubunge wa CCM katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Ukonga uliofanyika jana, Mwita Waitara ameibuka mshindi baada ya kupata kura ya asilimia 89.1.

Waitara ametangazwa mshindi leo tarehe 17 Septemba 2018 na Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Ukonga, Jumanne Shauri, ambapo msimamizi huyo alisema Waitara alipata kura 77,795.

Katika uchaguzi huo, mpinzani wa karibu alikuwa mgombea wa Chadema, Asia Msangi aliyeambulia kura 8,676 sawa na asilimia 9.95.

Wakati akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Shauri alisema waliopiga kura ni asilimia 29.4 kati ya watu 300,609 ya waliotarajiwa kupiga kura.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.