Polepole: CCM itaibuka mshindi Ukonga, Monduli

Polepole: CCM itaibuka mshindi Ukonga, Monduli

14 September 2018 Friday 15:30
Polepole: CCM itaibuka mshindi Ukonga, Monduli

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema chama chake kitashinda uchaguzi mdogo katika majimbo ya Ukonga na Monduli unaotarajia kufanyika Septemba 16, 2018.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Septemba 14, 2018 Polepole amesema CCM imefanya kampeni za kistaarabu na wananchi wamejitokeza kwa wingi kuwasikiliza.

"Tathmini ya awali inaonyesha kwamba mikutano yetu ya hadhara ilikuwa mikubwa mara tatu kuliko ile waliyofanya wenzetu," amesema.

Polepole amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi na kukichagua chama tawala li kiwaletee maendeleo kwenye maeneo yao.

"Wachague wagombea wa CCM ili wakawe kiungo na Serikali katika kutatua kero zao. Ukichagua mgombea wa CCM, atashirikiana na viongozi wa Serikali kuleta maendeleo," amesema.

Polepole amesema chama chake kinatoa elimu juu ya sheria za uchaguzi. Pia, amesema wanatoa elimu juu ya kanuni za uchaguzi za CCM.

Amesema katika awamu hii, CCM imejipanga kufanya siasa safi za kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo. Amesema chama chake kimejipanga kutatua kero mbalimbali.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.