Rais Magufuli awaita Wabunge wa upinzani kuwatua mizigo

Rais Magufuli awaita Wabunge wa upinzani kuwatua mizigo

27 September 2018 Thursday 13:40
Rais Magufuli awaita Wabunge wa upinzani kuwatua mizigo

RAIS John Magufuli amewakaribisha wabunge na madiwani wa upinzani wanaosumbuka na mizigo katika vyama vyao, kuingia CCM.

Rais Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, ameyasema hayo leo tarehe 27 Septemba 2018 jijini Dar es Salaam wakati akifungua barabara ya juu (Fly Over) katika makutano ya barababara ya Nyerere na Tazara.

Aidha, Rais Magufuli amewapongeza wabunge wanaotambua na kuunga mkono juhudi za serikali akiwemo Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.

“Ninawapongeza wabunge walioona mambo mazuri yanayofanywa na serikali akiwemo Waitara, sijasema wote waje siwahitaji, lakini wanaoguswa. Wanaosumbuka na mamizigo ya vyama vingine waje ninawakaribisha tuweze kujenga nchi yetu,” amesema.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.