Sakata la korosho, Mbunge anusa harufu ya ufisadi

"Hii inaenda kuwa kashfa kama ya EPA, Escrow, Richmond kwa unyenyekevu kama tulijikwaa basi tusiendelee bila kuwa na sababu ya msingi, ukweli tatizo lipo"

Sakata la korosho, Mbunge anusa harufu ya ufisadi

"Hii inaenda kuwa kashfa kama ya EPA, Escrow, Richmond kwa unyenyekevu kama tulijikwaa basi tusiendelee bila kuwa na sababu ya msingi, ukweli tatizo lipo"

21 May 2019 Tuesday 10:44
Sakata la korosho, Mbunge anusa harufu ya ufisadi

Na mwandishi wetu, Dodoma
MBUNGE wa Rombo, Joseph Selasini(Chadema) amemtaka spika wa Bunge  kuunda kamati maalum ya Bunge au ofisi ya CAG kuchunguza sakata zima la zao la  korosho.

Hatua yake hiyo ni kufuatia kuwepo kwa taarifa kuwa  korosho zimeoza katika maghala kwa asilimia 30.


Ameeleza hayo  leo Mei 21, 2019 Bungeni  mjini Dodoma alipokuwa akichangia hoja katika hotuba ya bajeti ya Wizara ya Kilimo.
 
Amesema hasara kubwa itapatikana endapo suala hilo likipuuzwa na kwamba Korosho inaoza kama vitunguu vinavyooza na kwamba maji  ya korosho yaliyooza yakigusa nyingine inaziozesha.

"Spika sisi(Bunge) ndio tunayoisimamia serikali, kama kuna ubishi kama korosho zimeoza au la tengeneza kamati ya watu wachache ikakague, ikaone wakuletea taarifa. Mimi(Selasini) ni muuzaji wa Korosho ninajua hili zao na tayari korosho zimeanza kuoza kwa asilimia 30 katika maghala na maji yaliyooza yakigusa nyingine zinaoza," amesema na kuongeza
"Taifa litapata hasara, watu watapata hasara kwa kuwa maghala yamejaa na msimu mwingine wa korosho unakuja.
"Hii inaenda kuwa kashfa kama ya EPA, Escrow, Richmond kwa unyenyekevu kama tulijikwaa basi tusiendelee bila kuwa na sababu ya msingi, ukweli  tatizo lipo na kama utaona haifai kwa kamati ya Bunge basi ofisi ya CAG ikakague matumizi ya fedha yalivyotumika na tumepata hasara kiasi gani."

Amesema anasikitishwa na jinsi masuala ya kitaifa yanavyofanyiwa  masihara na siasa.

Pamoja na mambo mengine ameiomba serikali kuhakikisha inavuna kwa kuyaifadhi maji ya mvua ambayo kwa sasa yanapotea bila kutumika katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo nchini.

Updated: 21.05.2019 12:45
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.