Uchaguzi serikali za mitaa kutumia bilioni 82

Uchaguzi serikali za mitaa kutumia bilioni 82

12 June 2019 Wednesday 09:26
Uchaguzi serikali za mitaa kutumia bilioni 82


Na mwandishi wetu, Dodoma
SERIKALI imesema takribani bilioni 82 zitatumika katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji nchini kote mwaka 2019.

Naibu waziri ofisi ya rais Tamisemi, Mwita Waitara amesema hayo leo Juni 12, 2019 Bungeni mjini Dodoma.

Amesema sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi huo utakaofanyika Oktoba zimeshakamilika na zilitangazwa rasmi mwezi Aprili mwaka huu.

Amevitaka vyama vya siasa kujiandaa kwa uchaguzi huo na kwamba kampeni bado hazijaanza.
"Uchaguzi wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji kwa mwaka 2019 utagharimu zaidi ya bilioni 82. Kanuni, taratibu na sheria tayari zimeshatangazwa. Utafanyika Oktoba, mwaka huu,'' amesema

Updated: 12.06.2019 09:34
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.