Vyama nane kumpinga rais Mahakamani

Ili chaguzi ziwe huru, tunaenda kufungua kesi mahakama kuu kupinga rais kuteua viongozi wa Nec, pia tutaendelea kupigania kupatikana kwa Katiba mpya

Vyama nane kumpinga rais Mahakamani

Ili chaguzi ziwe huru, tunaenda kufungua kesi mahakama kuu kupinga rais kuteua viongozi wa Nec, pia tutaendelea kupigania kupatikana kwa Katiba mpya

22 May 2019 Wednesday 12:48
Vyama nane kumpinga rais  Mahakamani


Na mwandishi wetu, Dar es salaam
 
UMOJA wa vyama  nane vya kisiasa nchini umepanga kufungua kesi ya kikatiba katika Mahakama kuu kupinga rais kuteua viongozi wa tume ya taifa ya uchaguzi(Nec).


Msimamo huo umetangazwa leo Mei 22, 2019 jijini Dar es salaam  na mwenyekiti wa umoja huo, Hashima Rungwe  katika mkutano wake na waandishi wa  habari na kwamba suala la upatikanaji wa katiba mpya utaendelea kupiganiwa.


"Ili chaguzi ziwe huru, tunaenda kufungua kesi mahakama kuu kupinga rais kuteua  viongozi wa Nec, pia tutaendelea kupigania kupatikana kwa Katiba mpya,'' amesema


Amedai kwa miaka mingi sasa CCM inashinda kwa mabavu katika chaguzi na inatumia mbinu nyingi ikiwemo watendaji mbalimbali wa serikali ambao amedai ni makada wa chama hicho.
"Ndio maana kuna wakati unajiuliza hivi hawa CCM wanashinda kwa mujibu wa sheria au mabavu,'' amesema


Msimamo huo unatolewa ikiwa ni wiki chache baada ya mahakama kuu kutoa hukumu ya kutaka kubadilishwa kwa kipengele  cha sheria kinachoruhusu  wakurugenzi wa halmashauri za wilaya, manispaa na majiji kuwa wasimamizi wa uchaguzi.
 
Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Atuganile Ngwala Mei 10,2019 kwenye kesi ya msingi namba 6 ya mwaka 2018 iliyofunguliwa na mtoto wa marehemu Chacha Wangwe ambaye ni Bob Chacha Wangwe.


Katika kesi hiyo ya Kikatiba, Jaji Ngwala alibatilisha vifungu viwili vya Katiba cha 7 (1) ambapo kinaeleza kuwa ‘Kila Mkurugenzi wa Jiji na Halmashauri wanakuwa wasimamizi wa Uchaguzi Mkuu


Pia ilibatilisha Kifungu cha 7 (3) kinachoeleza kuwa Tume inaweza kumchagua mtu yoyote kuwa msimamizi wa Uchaguzi wakati katiba inasema huwezi kuwa Mwanasiasa na ukawa msimamizi wa uchaguzi bali inatakiwa achaguliwe mtu huru.


Baada ya kueleza hayo, Jaji Ngwala alisema anazifuta sheria hizo na kama kuna upande haujaridhika ukate rufaa.
Umoja huo unaundwa na ACT Wazalendo, CCK, CHAUMMA, CHADEMA, DP, NCCR Mageuzi, NLD na UPDP

Updated: 23.05.2019 09:13
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.