Vyuma havijakaza, bali vimepinda asema Sumaye

Vyuma havijakaza, bali vimepinda asema Sumaye

13 September 2018 Thursday 19:41
Vyuma havijakaza, bali vimepinda asema Sumaye

Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amesema wananchi kama wataendelea kuichagua CCM, watarajie hali ngumu ya maisha.

Sumaye akihutubia mkutano wa kampeni wa Chadema wa uchaguzi mdogo jimbo la Ukonga leo, alisema: “Sasa hivi sio vyuma vimekaza tu bali vimepinda na hapo bado.”

 “Kama tutaendelea na hicho Chama Cha Mapinduzi hii hali tunayoisema mbaya hii ni trela tu, sinema bado mbaya."

“Tusipochagua chama cha upinzani tutazidi kuvumilia, mimi nilikuwa Waziri Mkuu lakini nilipoona tunakowapeleka Watanzania siko nilihamia upande wa pili ili kuwatumikia wananchi,” alisema.

Sumaye ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani aliwataka wananchi wa jimbo hilo wamchague Asia Msangi kupitia chama hicho ili uwe mwanzo wa dalili ya 2020 upinzani kuchukua nchi.

Naye Mwenyekiti Baraza la Wazee Chadema, Hashim Juma alisema:  “Imefika muda CCM ikae pembeni iwapishe waishike nchi.

“Wacha wao waende Dodoma, ila watuachie Ikulu yetu, Chadema tukichukua nchi tutarudi Dar es Salaam hapa ndiyo kwenye kila kitu,” alisema.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.