Wanadiplomasia 246 waswekwa Jela

"Mwendesha mashataka Mkuu wa serikali jijini Ankara amesema Maafisa hao wanaokamatwa ni wale wanaotuhumiwa kuwa na uhusiano wa karibu na Fethullah Gulen"

Wanadiplomasia 246 waswekwa Jela

"Mwendesha mashataka Mkuu wa serikali jijini Ankara amesema Maafisa hao wanaokamatwa ni wale wanaotuhumiwa kuwa na uhusiano wa karibu na Fethullah Gulen"

21 May 2019 Tuesday 12:06
Wanadiplomasia  246  waswekwa Jela


SERIKALI ya Uturuki imetoa amri ya kukamatwa kwa maafisa 246 wa Wizara ya Mambo ya Nje ambao wanadaiwa kuhusika na kuyasaidia makundi yanayolaumiwa na serikali hiyo kuhusika na jaribio la kuipindua serikali ya Recep Tayyip Erdogan Julai 15, 2016.


Kwa mujibu wa Mwendesha mashataka Mkuu wa serikali jijini Ankara amesema Maafisa  hao wa mambo ya nje wanaokamatwa  ni wale wanaotuhumiwa kuwa na  uhusiano wa karibu na mtandao wa kundi linalodaiwa kuongozwa na Fethullah Gulen mwanazuoni wa Kiislamu anayeishi mafichoni nchini Marekani


Shirika la habari la Serikali Anadolu Agency lilithibitisha tayari wafanyakazi 106 wanaotuhumiwa wameshakamatwa sehemu mbalimbali nchini humo kufikia jana jioni baada ya mwendesha mashtaka kuthibitisha kuwa walidanganya Wizara ya Mambo ya nje ya nchi hiyo kuwa walifaulu mitihani ya kuingia kwenye ajira hiyo serikalini


Viongozi wa Uturuki wamekuwa wakidai Mtandao wa Gulen umefanikiwa kupenyeza wafuasi wake kwenye serikali na jeshini na kuendesha mambo sambamba na serikali ili kutimiza ajenda zao za kisiasa Madai ambayo Gulen amekuwa akiyakanusha.


Zaidi ya watu 77000 wapo magerezani wakingojea kusikilizwa kwa kesi zao, huku 150,000 wakiwemo watumishi wa umma na wanajeshi, waalimu. Wanasheria,  Polisi na wamefukuzwa kazi na wengine kusimamishwa  kwa kuhusishwa na jaribio la Julai 2016.
 

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.