Zitto afunguka mazito kuhusu Tundu Lissu

Zitto afunguka mazito kuhusu Tundu Lissu

07 September 2019 Saturday 14:06
Zitto afunguka mazito kuhusu Tundu Lissu

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

MBUNGE wa Kigoma Mjini,Zitto Zuber Kabwe(ACT Wazalendo) amefunguka mazito katika ukurasa wake wa twitter juu ya shambulio la aliyekuwa Mbunge Tundu Antipas Lisu.

Leo Septemba 7. 2019 ,ndio tarehe na mwezi ambao Tundu Lisu alipigwa risasi na watu wanaoitwa wasiojulikana,siku hii imemfanya Zitto Kabwe kutokujizuia na ameandika maneno mazito huko twitter.

Ameandika tweets 10 ambazo nimekuletea hapa chini.

1." *Leo imetimia miaka 2* tangu shambulizi lililokusudia kumwua Mbunge mwenzetu Tundu Lissu. Tunamshukuru sana Mungu kwa uwezo wake na maajabu yake ambayo yamemweka hai mwenzetu na sasa amepona na kuweza kushiriki nasi katika mapambano ya kuhami na kukomaza demokrasia yetu."

2." *Siku ya Tarehe 7/9/2017* ilianza kama siku nyengine tu kwa Wabunge na Watanzania. Rais @MagufuliJP alikuwa Ikulu akizungumzia sarakasi za makanikia, Tundu akiwa Bungeni akitimiza majukumu yake kwa kujadili Azimio la Malawi-Tanzania ( Mto Songwe). Ilipofika saa 7/8 mchana mzizimo"

3." *Mapito ambayo alipita ndugu Lissu* siku hiyo hakuna mtu anatamani kupita. Nchi nzima ilitaharuki. Macho na masikio yakawa General Hospital Dodoma na baadaye Nairobi kisha Leuven, Belgium. Mbunge kushambuliwa na risasi saa saba mchana akiingia nyumbani haijapata kutokea TANZANIA"

4." *Haijapata kutokea pia tukio kama hilo kutochunguzwa* na vyombo vya Dola vyenye mamlaka ya uchunguzi. Miaka 2 sio tu hajakamatwa hata panzi, bali pia Tundu Lissu alinyimwa matibabu, kazushiwa kila aina ya propaganda na sasa kavuliwa ubunge. Ukatili ambao haumithiliki"

5. *Kabla ya tarehe 7/9/2017 binafsi nilikuwa nabadili Siasa* kwa imani kuwa labda utawala mpya una nia ya dhati kwa nchi yetu. Baada ya tarehe 7/9/2017 na haswa baada ya kumwona Tundu hospitali, niliazimia ndani ya nafsi yangu kuwa huu ni utawala KATILI kuliko zote TANZANIA

6. *Wenzangu waliniuliza mbona umekuwa mkali sana post Sept 7, 2017?* Nikawaambia kuwa lengo la waliomshambulia Lissu ni kutunyamazisha. Tukinyamaza watakuwa wameshinda. Sasa sote twapaswa kuwa Tundu Lissu ili kutowapa ushindi watu katili na dhalimu. Mwenendo wa Siasa ulibadilika

7. *Nimemwona Tundu akiwa kwenye matibabu mara 5*. Mara 2 Nairobi na mara 3 Ubelgiji ikiwemo ya juzi ambayo niliweza kutembea naye mtaani. Mungu ni mkubwa sana. Lakini pia Mungu hufanya baadhi ya maajabu yake kwa sababu maalumu. Naamini alimponya Lissu ili kuiponya demokrasia yetu

8. *Kuna watu hupenda kurudisha nyakati na kuonyesha kuwa Mimi na Lissu tulikuwa maadui*. Hatukuwa maadui Lakini pia hatukuwa na mwono mmoja kisiasa. Sote tumegundua tofauti zetu hazikuwa na msingi wowote na waliotufitini kama Dkt. Slaa sasa ni mabalozi wa utawala Katili.

9. *Mimi na Lissu tumeamua kwa dhati kufanya kazi pamoja kwa kuweka maslahi ya nchi yetu mbele*. Wanaoturudisha nyuma wakidhani watazuia umoja huu wanajisumbua. Nchi yetu ni kubwa zaidi ya zilizokuwa tofauti zetu. Kuhami na kukomaza demokrasia yetu ni kazi ya utukufu na TUTAIFANYA.

10. *Tunamwomba Mungu aendelee kutuweka hai tutimize wajibu wa kizazi chetu* kwa kuongoza mabadiliko makubwa ya kisiasa yatakayowezesha wananchi kuwa na maisha mazuri ya raha na furaha. Nawataka wana demokrasia wengine wote tutazame mbele. Nkrumah alisema *

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.