Zitto Kabwe ampa tano mbunge wa CHADEMA

Zitto Kabwe ampa tano mbunge wa CHADEMA

15 June 2018 Friday 17:45
Zitto Kabwe ampa tano mbunge wa CHADEMA

Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amempongeza Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Kigoma Upendo Peneza (CHADEMA) kuwa amefanikiwa kuacha alama ndani ya bunge la Tanzania akiwa na muda mfupi ndani ya bunge.

Amesema kuwa Peneza anaingia katika rekodi za Wabunge waliotumia nafasi yao kushawishi jambo lenye faida kubwa kwa jamii na likafanikiwa ikiwa ni baada ya Serikali kutangaza kuondoa kodi ya VAT kwenye Taulo za Kike zinazotumika na Wanawake kipindi cha hedhi.

“Kumekuwa na juhudi za kuleta mabadiliko haya miaka mingi kutokana na kazi za Mashirika kama TGNP Mtandao, SNV, Msichana Initiative nk. Upendo, licha ya kuwa na miaka miwili tu Bungeni ameweza kubeba hoja hii na kuiingiza Bungeni na kuunganisha Wabunge wote kutoka Vyama vyote.” amesema Zitto

Aidha, Zitto amesema kuwa Peneza sasa amepanda daraja kutoka kuwa mbunge na kuwa mwana Bunge, huku akisisitiza kuwa ameipa Bajeti ya mwaka 2018/19 taswira ya bajeti ya kijinsia.

Hata hivyo, kumekuwepo na kampeni ambayo imekuwa ikiendeshwa na taasisi mbalimbali inayokwenda kwa jina la ‘Namthamini’ kwa muda wa miaka miwili sasa.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.