Simba yaifunga KK Home Boys yaenda fainali Sports Pesa

Simba yaifunga KK Home Boys yaenda fainali Sports Pesa

07 June 2018 Thursday 13:51
Simba yaifunga KK Home Boys yaenda fainali Sports Pesa

KUMEKUCHA NAIROBI: Jonas Mkude aipeleka Simba fainali Sports Pesa

KUMEKUCHA NAIROBI: Jonas Mkude aipeleka Simba fainali Sports Pesa

Na Mwandishi Wetu, Nairobi

Kiungo wa Mabingwa wa soka wa Tanzania Bara, Jonas Mkude ameipeleka timu ya Simba SC fainali baada ya kufunga mkwaju wa penati ya mwisho dhidi ya Kakamega maarufu kama KK Home Boys katika nusu fainali ya kwanza ya michuano ya Sports Pesa.

Simba ilifanikiwa kufunga mikwaju yote ya penati ambayo yalifungwa na Haruna Niyonzima, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Shzia Kichuya na Jonas Mkude.

Mpaka kipindi cha pile kinakamilika hakuna timu yeyeyote ambayo imepata goli.

Michuani hiyo ilifanyika kwa mara ya kwanza mwaka jana hapa nchini na klabu ya Gor Mahia kuibuka mabingwa na kujipatia fursa ya kucheza na Everton ya Uingereza ndani ya ardhi ya Tanzania.

Vilabu vya Tanzania hasa Simba vimeonesha kuyapa umuhimu mkubwa mashindano hayo msimu huu zaidi ya msimu uliopita.

Swali linabaki je, Simba itafanikiwa kuliokoa jahazi hili la Tanzania, na kwenda Uingereza kucheza Everton jijini Liverpol.

Hata hivyo, Simba itaweza kukutana na ndugu zao wa Singida United ambao wanacheza jioni hii katika nusu fainali ya pili dhidi ya Gol Mahia ya jijini Nairobi.

Azania Post

Azania Post

Updated: 07.06.2018 15:29
Keywords:
Tanzania
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.