banner68
banner58

Unai Emery kocha mpya wa Arsenal

Emery mwenye umri wa miaka 46 amejiunga na Arsenal baada ya kuondoka PSG

Unai Emery kocha mpya wa Arsenal

Emery mwenye umri wa miaka 46 amejiunga na Arsenal baada ya kuondoka PSG

23 May 2018 Wednesday 12:39
Unai Emery kocha mpya wa Arsenal

Klabu ya Arsenal imethibitisha kumteua Unai Emery kuwa kocha mpya wa klabu hiyo akichukua nafasi ya Arsene Wenger ambaye amestaafu baada ya kuitumikia Arsenal kwa miaka 22.

Emery mwenye umri wa miaka 46 amejiunga na Arsenal baada ya kuondoka Paris Saint-Germain ambapo aliingoza klabu hiyo kushinda ubingwa wa ligi kuu ya Ufaransa League 1.

Kocha huyo raia wa Hispania amesaini mkataba wa miaka miwili kutumikia Arsenal.

Afisa mkuu mtendaji wa klabu ya Arsenal, Ivan Gazidis amesema kocha huyo amekuwa na rekodi bora katika kazi yake na ana mtindo mzuri wa uchezaji mpira utakaoifaa Arsenal.

Arsenal wameshindwa kumaliza katika nafasi nne za juu msimu huu kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza huku wakitolewa kwenye kombe la Europa League katika hatua ya nusu fainali.

Unai Emery ana rekodi nzuri katika michuano ya Ulaya kwani ameshinda  makombe 3 mfululizo ya Europa aliyobeba akiwa na Sevilla mwaka 2014 waliifunga Benfica kwa penati, 2015 wakaifunga Ukrainians Dnipro kisha wakaipiga Liverpool 2016.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
owiye salim 2018-05-27 08:04:44

welcome

Avatar
juma timbalaida 2018-05-28 22:18:01

safitu