Yanga kuvuna pesa za usajili wa Mzambia Obrey Chirwa

Yanga kuvuna pesa za usajili wa Mzambia Obrey Chirwa

16 June 2018 Saturday 14:54
Yanga kuvuna pesa za usajili wa Mzambia Obrey Chirwa

Na Amini Nyaungo

Yanga inategemea kuvuna pesa za usajili wa Obrey Chirwa mara baada ya dili la nyota huyo kuonekana linakaribia kutimia moja ya timu inayoshiriki ligi kuu ya Misri.

Chirwa ametumia ukurasa wake wa Instagram kuonesha picha moja ya watu wanaosadikika kuwa ni mchezaji  wa klabu moja huko Misri ambayo jina la klabu hiyo bado halijafahamika.

Kwa taarifa hii inaonesha dhahiri kuwa Simba watakosa huduma ya mchezaji huyo ambapo taarifa zinaeleza kuwa kamati ya usajili ya Mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara walikuwa katika mazungunza makali ya kumsajili mchezaji huyo ambaye mkataba wake unakaribia kuisha.

Endapo Yanga watamuuza Chirwa watafaidika kwa kiasi cha usajili kwa kuwa bado hajamaliza mkataba wake.

Azania post imemtafuta afisa habari wa Yanga Dismas Ten amesema kuwa bado hawana taarifa yoyote ya mchezaji huyo kufichwa Misri licha ya kuna timu tatu zinamuhitaji.

Baada ya Chirwa kuposti picha katika ukurasa wake wa Instagram kumekuwa na maoni na huzuni kwa baadhi ya mashabiki wanaosadikika ni wa Yanga wakiamini bado anahitajika ndani ya Yanga.

Updated: 16.06.2018 16:52
Keywords:
Yanga
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Shafiq bin mbonjoro 2018-06-16 16:04:27

Nikweli ametusaidia sana ila sasa yanga inahitaji wachezaji wengine wenye moyo mmoja wakuitumikia yanga kwa mafanikio,kwaheri obrey cholla chirwa uko uendako tutakukumbuka kwa mema pia uliyofanya ukiwa yanga

Avatar
DASE 2018-08-01 19:49:23

SILASI