Yanga yatoa takrima kenya Sportpesa Super cup

Metheo Anthony kwa upande wa Yanga alifunga goli la kuwatia matumaini wapenzi wake dakika ya 39 ya mchezo, huku kipindi cha kwanza kiliisha matokeo...

Yanga yatoa takrima kenya Sportpesa Super cup

Metheo Anthony kwa upande wa Yanga alifunga goli la kuwatia matumaini wapenzi wake dakika ya 39 ya mchezo, huku kipindi cha kwanza kiliisha matokeo...

03 June 2018 Sunday 15:07
Yanga yatoa takrima kenya Sportpesa Super cup

Na Amini Nyaungo

BAADA ya kutoa takrima kwa timu za ligi kuu Tanzania bara klabu ya Yanga imeendelea kuwaonjesha namna gani walivyo vibaya ndani ya timu wakazi wa Nairobi baada ya kukubali kufungwa mabao 3-1 dhidi ya Kakamega Homeboys katika masindano ya  Sportspesa Super Cup.

Magoli mawili ya Kakamega yalipatikana kipindi cha kwanza cha mchezo yaliyofungwa na Allan Wanga dakika ya 26 baada ya kuwahadaa mabeki wa Yanga la pili amelifunga kwa mkwaju wa penati dakika ya 31.

Metheo Anthony kwa upande wa Yanga alifunga goli la kuwatia matumaini wapenzi wake dakika ya 39 ya mchezo, huku kipindi cha kwanza kiliisha matokeo yakiwa Kakamega 2 Yanga 1.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Yanga wakitaka kubadili matokeo ndipo dakika ya 86 wakajisahau Kakamega wakapiga ‘Counter attack’ na Opondo alipozamisha jahazi la Yanga.

Filimbi ya mwisho Yanga 1 Kakamega 3, bingwa wa michuano hii ataelekea England kucheza na Everton.

Azania Post

Updated: 03.06.2018 15:29
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.