Afungwa jela maisha kwa kuwaua wazazi wake kwa shoka

Afungwa jela maisha kwa kuwaua wazazi wake kwa shoka

07 June 2018 Thursday 16:43
Afungwa jela maisha kwa kuwaua wazazi wake kwa shoka

Mahakama nchini Afrika Kusini imemhukumu kifungo cha maisha jela mwanaume mwenye umri wa miaka 23 baada ya kumkuta na hatia ya kuwaua kwa kutumia shoka wazazi wake wote wawili pamoja na kaka yake.

Henri Van Breda, aliongezewa kifungo kingine cha miaka 15 kwa kosa la kujaribu kumuua mdogo wake wa kike, Marli, alipofanya shambulizi hilo Januari 2015.

Jaji Siraj Desai wa Mahakama Kuu, akisoma hukumu hiyo alisema kuwa Breda alifanya mauaji ya kikatili na shambulizi la kijambazi dhidi ya familia yake.

Mmoja kati ya mashahidi wa kesi hiyo ambaye ni mfanyakazi wa kitengo cha dharura, alisema kuwa tukio hilo lilikuwa baya zaidi kuwahi kushudia katika miongo minne aliyofanya kazi hiyo.

Henri Van Breda

Dar24 wamesema kuwa akiwa na umri wa miaka 20 wakati huo, Van Breda alitumia shoka kumchinja mama yake mzazi, Teresa akiwa na umri wa miaka 55, baba yake Martin mwenye miaka 54 na kaka yake Rudi aliyekuwa na umri wa miaka 22.

Alifanya mauaji hayo wakati ambapo familia hiyo ilikuwa imelala.Van Breda alikana kufanya kitendo hicho akidai kuwa yeye pia alikuwa mhanga wa tukio hilo kwani kuna mtu mwingine aliyevunja nyumba na kuishambulia familia hiyo kwa shoka.Mwanasheria wake amedai kuwa watakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Updated: 07.06.2018 16:45
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.