banner68
banner58

Ali Kiba amponza Ray Vany kwa Bill Nass katika 'pochi nene remix’

Ali Kiba amponza Ray Vany kwa Bill Nass katika 'pochi nene remix’

24 May 2018 Thursday 13:52
Ali Kiba amponza Ray Vany kwa Bill Nass katika 'pochi nene remix’

Na Amini Nyaungo

Ray Vany wa Wasafi Classic Baby (WCB) ametoa ngoma yake mpya ya ‘remix’ yake ya Pochi nene ambayo amewashirikisha mastaa wengi katika ngoma hiyo

Swali ambalo kila mmoja anjiuliza kwanini msanii Bill Nass ameachwa katika ‘collabo’ hiyo ambapo alionekana wakiwa studio huku akifanya baadhi ya mistari iliyosikika amekifanya vizuri.

Mdahalo huo umekuwa mkubwa imefika hatua hadi wengine wanasema ametolewa katika ngoma hiyo kwa kuwa  kambi pinzani.

Bill Nas anaukaribu na Ali Kiba na imekuwa rahisi kwake kumpongeza mkali huyo wa ‘Mvumo wa radi’ pindi anavyofanya vizuri.

Wengine wanasema labda kwa mistari iliyosikika aktaja baadhi ya viungo vya mkono inakumbusha tukio lake na msanii Nandy la kutoa video chafu heudna ndio sababu ya kukatwa katika ngoma hiyo.

Lengo la kuirudia nyimbo iwe kali zaidi ya ile ya mwanzoni ambayo  kama itakuwa haina ukali ule amba wengi wanautarajia basi mashabiki watakushusha.

Ray Vany tayari ameitoa ngoma hiyo huku akiwashirikisha wasanii wengi ambao wanafahamika wakikutana pamoja

Wasanii aliyowashirikisha ni Khaligraph Jones, Godzilla, Rosa Ree, Izzo BiznesS, Country Boy, Young Dee na Wakorinto.

Azania Post

Updated: 24.05.2018 14:13
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
243894006169 2018-10-11 22:22:13

454923