Bajeti Kuu: Wabunge washangilia kufutwa kodi taulo za kike 

Bajeti Kuu: Wabunge washangilia kufutwa kodi taulo za kike 

14 June 2018 Thursday 17:01
Bajeti Kuu: Wabunge washangilia kufutwa kodi taulo za kike 

Na Mwandishi Wetu

WABUNGE wameupokea kwa shangwe uamuzi wa serikali kufutwa kwa kodi ya ongezeko la thamani kwenye taulo za kike  kulikotangazwa jioni hii na waziri wa fedha na mipango Dk Philip Mpango.

Akisoma bajeti kuu ya serikali ya mwaka 2018/19 mjini Dodoma  Dk Mpango alisema kuwa ni matarajio yake wazalishaji watauza taulo hizo kwa bei nafuu sana.

Aidha alisema kuwa serikali pia imesamehe ongezeko la kodi kwenye vifungashio vya madawa ya binadanu vinavyozalishwa na viwanda vya ndani  kwa lengo la kupunguza gharama za uzalishaji na kulinda viwanda vya ndani

Alisema kuwa serkali pia imesahe kodi ya ongezeko la thamani kwenye virutibisho vya vyakula  vya mifugo toka nje kwa lengo la kuimarisha ufugaji bora.

Pia alipendekeza kuanzishwa kwa kodi za mfumo wa stempu za kielektoniki ambao  utasaidia  serikali kudhibti kodi,  mfumo unatumika ,Kenya , Moroko na Switezerland .

Updated: 14.06.2018 17:04
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.