Bungeni Dodoma: Maelfu ya wahamiaji haramu wakamatwa Tanzania

Bungeni Dodoma: Maelfu ya wahamiaji haramu wakamatwa Tanzania

29 May 2018 Tuesday 13:11
Bungeni Dodoma: Maelfu ya wahamiaji haramu wakamatwa Tanzania

Na Mwandishi Wetu

Bunge la Tanzania limeelezwa kuwa kuanzia mwezi Julai mwaka jana hadi Machi mwaka huu jumla ya wahamiaji haramu 13, 593 walikamatwa nchini.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni,wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Farhia Shomari (CCM).

Alisema kuwa wengi wao walipelekwa mahakama ambapo kuna kesi 2,363 , wengine kuachiwa na  wapo waliorudishwa makwao pamoja na kufungwa.

 Aliwataka wananchi wote wanaojiusisha na kuwasaidia wakimbizi hao kuingia nchini kuacha vitendo hivyo na kuwa serikali itawachukulia hatua kali

Masauni alisema kuwa watoto wa wahamiaji haramu wanaozaliwa nchini hawana haki ya kuwa raia kwa sababu ya wazazi wao waliingia nchini kwa njia kinyume na sharia.

Hata hivyo, Mbunge Shomari alitakakujua kama wahamiaji haramu wanapoingia nchini na kubahatika kupata watoto wanakuwa ni raia wa nchi gani.

Naibu Waziri Masauni alisema kuwa kwa mujibu wa sheria wakimbizi haramu wakiingia nchini na kubahatika kupata watoto hao huwa nao ni haramu.

Alisema kwa mujibu wa sheria angalau mzazi mmoja anatakiwa kuwa raia wakati mtoto huyo  anazaliwa  ndiyo anaweza kupewa uraia wa kuzaliwa.

Azania Post

Updated: 29.05.2018 13:54
Keywords:
Tanzania
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.