Bungeni Dodoma: Serikali yasitisha zoezi la upandishaji hadhi barabara

Bungeni Dodoma: Serikali yasitisha zoezi la upandishaji hadhi barabara

30 May 2018 Wednesday 14:11
Bungeni Dodoma: Serikali yasitisha zoezi la upandishaji hadhi barabara

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imesema kuwa imesitisha zoezi la kupandisha hadhi barabara za wilaya kuwa mkoa na sasa kazi hiyo itakuwa inafanywa na Wakala wa Barabara Vjijiji (Tarura).

Hayo yamesemwa bungeni leo na Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kwandikwa wakati alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Mchinga Hamidu Bobali (CCM) .

Mbunge huyo alisema kuwa Rais John Magufuli alipokuwa kwenye kampeni aliahidi kupandisha hadhi barabara moja wilayani Lindi na kuwa ya Mkoa na akaitaka serikali kueleza lini itafanya hivyo.

Akijibu , Naibu Waziri Kwandikwa, alisema kuwa Tarura ilianzishwa kwa ajili ya kutoa msukumo wa kuharakisha maendeleo.

Alisema kuwa kwa sasa zoezi la upandishaji hadhi wa barabara za wilaya kuwa za mkoa utafanywa na Tarura badala ya Tanroads.

Kuhusu ahadi za Rais , alisema kuwa zote zinajulikana na serikali itahakikisha zinatekelezwa ndani ya kipindi cha miaka mitano.

Akielezea kuhusu barabara  kutoka eneo ya Redio habari maalum hadi hospitali ya Arusha, Naibu Waziri huyo alisema kuwa serikali itaendelea na utaratibu wa kuirekebisha na ataitembelea kwa ajili ya kushauriana na mbunge wa Viti Maalum , Amina Mollel (CCM).

Kwandikwa amedokeza kuwa kwa ujumla wanatambua na kuboresha  barabara za mikoa ya Kusini kutokana na umuhimu wake.

Alisema kuwa maeneo hayo yanazalisha korosho , na serikali itayatazama kwa macho mawili na tayari imeanza kutengeneza barabara wilaya Newala kwa kiwango cha lami kipande cha urefu wa kilomita tatu.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.