Dkt. Hellen Kijo-Bisimba awakana Chadema

Dkt. Hellen Kijo-Bisimba awakana Chadema

01 June 2018 Friday 18:13
Dkt. Hellen Kijo-Bisimba awakana Chadema

Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha LHRC, Dkt. Hellen Kijo-Bisimba amekanusha taarifa ambazo zimezagaa katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kuwa ameteuliwa kujiunga na baraza la wazee wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media ambapo amesema kuwa hajapokea taarifa yeyote kutoka Chadema hivyo hawawezi kutangaza kitu kama hicho bila ya kumuuliza.

Amesema kuwa taarifa hizo ni za uzushi na wananchi wanapaswa kuzipuuza kwani yeye hana sifa za kuwa mwanasiasa na hata kama angechaguliwa asingekubali kuwa miongoni mwa baraza la wazee wa Chadema.

“Taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa nimechaguliwa katika baraza la wazee wa Chadema ni uongo, na hata kama ningechaguliwa nisingekubali,”amesema Dkt. Hellen Kijo- Bisimba

dar24.com

Updated: 01.06.2018 19:57
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.