Haji Manara akubali Simba kutobolewa tundu

Haji Manara akubali Simba kutobolewa tundu

24 May 2018 Thursday 14:29
Haji Manara akubali Simba kutobolewa tundu

Na Mwandishi Wetu

Msemaji Mkuu wa Simba Haji Manara amekubali kauli ya Rais John Pombe Magufuli aliyoisema dhidi ya timu ya Kagera Sugar juu ya kutobolewa tundu mbele ya mashabiki wao katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara.

Simba ilihitaji kuweka historia ya kucheza michezo 30 bila ya kufungwa ambapo ndoto yake ilizimwa na Kagera Sugar baada ya Simba kukubali kufungwa goli 1-0 goli lililofungwa na mchezaji wao wa zamani Edward Christopher.

Katika mchezo huo ulihudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kama mgeni rasmi, ambapo baada ya mechi aliwaambia mashabiki wa Simba waliojitokeza uwanjani hapo kuwa Kagera wameweza kutoboa tundu.

"Kagera wamefanikiwa kutoboa tundu mbele ya mashabiki wa Simba waliojitokeza hapa leo," amesema.

Naye Haji Manara amekubali huku akiwatania upande wa Yanga kuwa kweli wametobolewa tundu lakini yanga wamezidi kuwa na nyufa maana imezidi matundu.

"Sawa tumebolewa tundu, ila matundu ya Yanga yamezidi,"amesema.

Ligi kuu ya soka Tanzania bara inaisha jumatatu ya wiki ijayo ambapo Yanga itamaliza na Azam katika uwanja wa Tuafa Dar es Salaam.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.