banner58

Israel yaliangamiza kundi la Hamas usiku kwa makombora

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas alisema hatua ya Israel kulipiza kisasi mashambulizi hayo inaashiria kuwa Israel haitaki Amani.

Israel yaliangamiza kundi la Hamas usiku kwa makombora

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas alisema hatua ya Israel kulipiza kisasi mashambulizi hayo inaashiria kuwa Israel haitaki Amani.

30 May 2018 Wednesday 14:41
Israel yaliangamiza kundi la Hamas usiku kwa makombora

Na Mwandishi Wetu

KUNDI la Hamas limepokea kipigo kikali leo Usiku kutoka kwa jeshi la Israel baada ya mashambuliz ya makombora kuelekea kwenye maeneo 25 ya kundi hilo.

Imeripotiwa kuwa majibizano hayo yamezusha uwezekano wa kutokea tena vita vingine katika Ukanda huo wa Kipalestina unaodhibitiwa na vuguvugu la itikadi kali la Hamas, ambavyo vinaweza kuwa vya nne tangu mwaka wa 2008.

Jeshi la Israel limesema liliyalenge maeneo zaidi ya 60 ya kijeshi katika Ukanda wa Gaza katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita, ikisema karibu makombora 70 yalivurumishwa katika ardhi yake siku nzima ya Jumatatu, ambapo kadhaa yalizuiwa na mifumo ya ulinzi wa makombora ya angani.

Baada ya hali kuongezeka, ikifuatiwa na milio ya ving'ora na milipuko usiku kucha, kukawa na madai ya Wapalestina ya kufikiwa makubaliano ya kusitisha mapigano.

Jana usiku, msemaji wa kundi la Islamic Jihad ambalo ndilo la pili kubwa lenye silaha katika Ukanda wa Gaza baada ya Hamas, alisema makubaliano ya kuweka chini silaha yamefikiwa, na leo afisa wa ngazi ya juu wa Hamas Khalil al-Hayya akazungumzia muafaka huo.

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas alisema hatua ya Israel kulipiza kisasi mashambulizi hayo inaashiria kuwa Israel haitaki Amani.

Kumekuwa na utulivu kiasi leo asubuhi katika Ukanda wa Gaza. Machafuko ya jana yalifuatia wiki za vurugu na maandamano kwenye mpaka kati ya Israel na eneo la Kipalestina linalozingirwa. Baraza za usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kukutana leo kuyajadili machafuko hayo ya Gaza, kufuatia ombi la Marekani la kuandaliwa mkutano wa dharura.

Azania Post

Updated: 30.05.2018 14:59
Keywords:
Israel
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.