Jeuri ya Pesa: Mchezaji wa Simba Shiza Kichuya kutua Azam

Jeuri ya Pesa: Mchezaji wa Simba Shiza Kichuya kutua Azam

07 June 2018 Thursday 12:57
Jeuri ya Pesa: Mchezaji wa Simba Shiza Kichuya kutua Azam

Na Amini Nyaungo

Jeuri ya pesa hukomeshwa na pesa ndio kauli ya mashabiki wa Simba na Azam wanavyotambiana hivi sasa baada ya uongozi wa Azam kuhitaji huduma ya Shiza Kichuya.

Taarifa ambazo zisizo rasmi zinasema matajiri wa Azam wanamuhitaji kwa udi na uvumba nyota wa Simba, Shiza Kichuya kwa ajiri ya kutengeneza Azam mpya msimu ujao.

Wiki iliyopita msemaji  mkuu wa Simba Haji Manara alinukuliwa akisema wameshamalizana na nyota huyo kwa ajiri ya msimu ujao, huku leo zikiibuka tetesi za nyota huyo kuelekea Azam.

Pia kuna taarifa za kutakiwa TP Mazembe ya Kongo.

Kichuya ambaye ametokea Mtibwa Sugar alijiunga na Simba 2016 akiwa mfungaji bora wa timu hiyo kwa kufunga magoli 12 , msimu ulioisha ameweza kufunga magoli 8 na kutoa nafasi 7 za magoli.

Ni mchezaji tegemeo wa Simba ana madhara makubwa endapo ataondoka bado itaiathiri klabu hiyo ambayo imetawadhwa kuwa mabingwa wa ligi kuu bara 2017-2018.

Azania Post

Updated: 07.06.2018 15:45
Keywords:
Simba SCAzam
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.