Kufuru Mapokezi ya Diamond Platnumz Tandale

Kufuru Mapokezi ya Diamond Platnumz Tandale

16 June 2018 Saturday 19:28
Kufuru Mapokezi ya Diamond Platnumz Tandale

Na Mwandishi wetu,

Nguli wa muziki wa Bongo Flavor, Nassib Abdul maarufu kama Diamond Platnumz jana alipokelewa kwa kufuru na umati wa wakazi wa Tandale wakati alipowatembelea kwa lengo la kutoa mkono wa Eid Eil-Fitr.

Diamond alitangaza kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa atasherekea siku kuu hiyo kubwa ambayo ni moja ya nguzo tano za Kiislamu duniani kote pamoja na wakazi wa Tandale ambapo ndipo alipozaliwa.

“Najisikia furahaa sana, kwanza sikutegemea kabisa kama kutakuwa na umati huu. Nilitangaza tu kwenye ukurasa wangu wa Instagram lakini ni ajabu kwa umati huu mkubwa.

“Nafurahi kuwa Tandale, hapa ndipo nilipozaliwa, hawa wote ni watu wangu na wazee hawa ni marafiki zangu nilikulia hapa nikiwa chini ya busara zao na malezi yao,” alisema Diamond.

Diamond likuwa chini ya ulinzi mkali wa mabaunsa wake ambao walikuwa wamemzingira kila upande ingawa hawakumzuia alipotaka kuongea na wazee, watoto na kinamama aliowazoea katika mtaa huo maarufu kama Tandale.

Azania Post

Updated: 16.06.2018 20:31
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.