Kutoka Bungeni: Mbunge CCM ataka maonyesho nane nane yasifanyike Dodoma

Kutoka Bungeni: Mbunge CCM ataka maonyesho nane nane yasifanyike Dodoma

07 June 2018 Thursday 11:44
Kutoka Bungeni: Mbunge CCM ataka maonyesho nane nane yasifanyike Dodoma

Na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Viti Maalum Mariam Nassoro Kisangi (CCM) ameitaka serikali kuyahamisha  maonyesho ya wakulima nane nane yanayofanyika kikanda Mkoani Dodoma kwani kwa sasa limekuwa jiji.

Alikuwa akiuliza kwenye kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu, ambapo alisema kuwa kukiwa na jiji shughuli za kilimo zinapungua sana na hivyo akaitaka serikali kuipa fursa mikoa mingine

Aliyataja majiji ya Tanzania kuwa ni pamoja na Mbeya, Arusha ,Mwanza na Dar es Salaam ambapo alisema kuwa shughuli hizo zimepungua sana.

Akijibu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alisema maonyesho ya wakulima nane nane yanatoa fursa kwa watanzania kuonyesha kazi za kilimo.Alisema kuwa Wizara  ya Kilimo  imepewa jukumu ya kuratibu maonyesho hayo kikanda  na ndiyo yenye maamuzi kuhusu eneo la kufanyika.

Alisema kuwa kuhusu kuhamisha maonyesho ya wakulima Dodoma, uamuzi upo kwa Wizara  hiyo wao wanaweza kuyapeleka mkoa jirani hata wa Singida

Alidokeza kuwa yeye amewahi kuwa mgeni rasmi wa maonyesho ya wakulima nane nane Mkoani Mbeya na haoni kama ni sheria lakini mamlaka hayo ni ya kikanda.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo lengo la maonyesho hayo ni kuhakikisha kuwa huduma zinapatikana, na watu wanatumia utafiti mbali mbali kulingana na mazingira kwa ajili ya kuinua kilimo.

Aidha Majaliwa alisema kuwa Waziri wa Kilimo amesikia na kama kuna umuhimu wa kufanya hivyo basi yeye ndiyo mwenye jukumu hilo.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.