Kutoka Bungeni: Serikali yaua mamia ya ngedere wasumbufu

Kutoka Bungeni: Serikali yaua mamia ya ngedere wasumbufu

29 June 2018 Friday 12:29
Kutoka Bungeni: Serikali yaua mamia ya ngedere wasumbufu

Na Mwandishi Wetu

ZAIDIya ngedere 100 wameuawa huko wilaya ya Bukoba vijijini baada ya kuonekana wanawasumbua wananchi na kusababisha madhara makubwa.

Hayo yamesemwa bungeni leo na Naibu Waziri wa Mali Asili na Utalii Japhet Hasunga wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti maalum (CUF) Alfredina Kahigi.

Mbunge huyo alitaka kujua mikakati ya serikali ya kuondokana na balaa la wanyama aina ya ngedere ambao wamekuwa wakivamia wanavijiji huko Bukoba Vijijini .

Alisema kuwa wanyama hao wanawavamia wanavijiji na kusababisha madhara na kuitaka serikali kuendeleza mkakati wake dhidi ya balaaa hilo.

Akijibu swali hilo , Naibu Waziri Hasunga alisema kuwa serikali inatambua uwepo wa wanyama waharibifu katika wilaya 80 nchini. Awalitaja wanyama waharibifu hao kuwa ni tembo, mamba na ngedere .Alifafanua kuwa tembo wanavamia mashamba ambapo mamba na ngedere wanajeruhi wananchi katika maeneo ya Kemondo, Kizi, Katangarara Katoma  Bujogo na Kishongo.

Alisema kuwa wizara imekuwa ikifanya doria kwa kushirikiana na askari wa wanyama pori kutoka Mwanza. Alidokeza kuwa kwa kushirikiana na askari wa Pori la Burigi jumla ya ngedere  103 waliuawa katika maeneo zaidi ya saba katika vijiji hivyo. Alikiri kuwa kuna uhaba wa askari wa wanyama pori na kuongeza kuwa serikali itaendelea kushirikiana na mamlaka husika kuhakikisha kuwa wanyama hao wanadhibitiwa.

Alisema kuwa vifaa havitoshi kuwadhibiti wanyama hao lakini nia ya serikali ni kuona kuwa inaongeza na kuwa na vya kisasa ikiwemo matumizi ya ndege zisizotumia rubani.

Hata hivyo alisema kuwa hawashauri watu kuwaua wanyama pori kwani wana haki ya kuishi.Alidokeza  kuwa pale inapobainika wamekuwa wengi kuna utaratibu wa kuwavuna kwa njia endelevu lakini haishauri kuwaua.

Kuhusu migogoro kwenye hifadhi., alisema kuwa tayari wamekwisha jipanga ambapo Waziri mwenye dhamana, Dk Hamis Kigwangalla atatembelea maeneo yote ikiwamo Urambo mkoani Tabora.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.