Kutoka Bungeni: ‘Tiba’ wahamiaji haramu yapatikana

Kutoka Bungeni: ‘Tiba’ wahamiaji haramu yapatikana

29 May 2018 Tuesday 12:26
Kutoka Bungeni: ‘Tiba’ wahamiaji haramu yapatikana

Na Mwandishi Wetu

TATIZO la wahamiaji wanaokamatwa nchini Tanzania huenda likaisha mara baada ya nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki kukubaliana kuwauzia kwenye mipaka wanayoanzia.

Hayo yamesemwa bungeni leo na Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Fatma Tawfiq (CCM) .

Mbunge huyo alisema kuwa tatizo la wahamiaji haramu kutoka nchini Ethiopia wanaokamatwa Tanzania limekuwa linaongezeka na kuna haja kwa serikali kuongea kidiplomasia na nchi husika kwa kuweka utaratibu maalum ili kulipungizia gharama taifa letu.

Akijibu swali hilo, Waziri Nchemba, alisema kuwa wiki iliyopita walikuwa na vikao na jumuiya ya Afrika Mashariki na wakaazimia na kupitisha baadhi ya mambo.

Alisema kuwa wamekubaliana kuoanisha sheria kwa kuzikataza nchi za Kenya na Sudan kusini kupitisha wahamiaji haramu hao kwenye nchi zao.

Alisema kuwa wahamiaji hao wamekuwa wakipita nchi hizo bila kipingamizi  na kuanzia sasa watakuwa wakizuiwa kuendelea na safari hadi kupata vibali halali.

Wakati huo huo, Mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa alisema kuwa tatizo la wahamiaji haramu ni kubwa huku akitolea mfano wa gereza la Ruanda la Mbeya ambalo wapo 41 ambao wamemaliza vifungo vyao lakini serikali imeshindwa kuwarudisha makwao.

Akijibu Swali hilo,  Naibu waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni, alisema kuwa  serikali itafana jitihada za kuwarudisha wahamiaji hao kwa kushirikina na shirika la kimataifa la uhamiaji la IOM.Alisema kuwa serikali haipendi wahamiaji hao kuendelea kuishi gerezani wakati wamemaliza vifungo vyao, hata hivyo matatizo kama hayo yapo sehemu chache.

Azania Post

Updated: 29.05.2018 12:56
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.