banner68
banner58

Makonda: Wababa 295 wakubali kulea watoto waliowatelekeza

..atawachukulia hatua za kisheria  wale wanaume waliokataa wito wake ambao wanakadiriwa kufikia 107

banner57

Makonda: Wababa 295 wakubali kulea watoto waliowatelekeza

..atawachukulia hatua za kisheria  wale wanaume waliokataa wito wake ambao wanakadiriwa kufikia 107

14 April 2018 Saturday 11:35
Makonda: Wababa 295 wakubali kulea watoto waliowatelekeza

Na Mwandishi Wetu

IDADI ya watoto wa mitaani wanaoishi jiji la Dar es Salaam kwa sababu  mbali mbali ikiwemo  migogoro ya familia kwa sasa imefikia zaidi ya 5,000 Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda amesema.

Akizungumza mapema leo Jumamosi kuhusu tathimini ya zoezi la kuwasaidia wanawake wenye matatizo ya ndoa na ambao wametelekezwa  na wenza wao, Bw Makonda alisema kuwa idadi hiyo ni kubwa na kuna umuhimu  wa kuangalia uwezekano wa kupambana na changamoto hiyo.

Alisema kuwa idadi hiyo inaonyesha jinsi ukubwa wa tatizo hili  na  kuomba ushirikiano kwa wazazi au ndugu kuweza kuwaokoa watoto hao.

“Ninashukuru hadi sasa kuna akiba baba 295 ambao wamekubali kuwalea watoto wao waliowatelekeza kwa muda mrefu”, alisema,

Alisema kuwa zoezi hilo kwa kiasi limefanikiwa na kuongeza kuwa  atawachukulia hatua za kisheria  wale wanaume waliokataa wito wake ambao wanakadiriwa kufikia 107.

Kwa mujibu wa Makonda hadi sasa, wabunge waliotajwa ni 47 huku viongozi wa dini ni 14. Aidha katika orodha hiyo anadaiwa kutajwa pia mmoja wa wanasiasa ambao walijitokeza kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Kuhusu kutajwa kwa viongozi wa kisiasa na kidini katika tukio hilo, Makonda alisema inasikitisha kuona kuwa hata viongozi wa kisiasa na dini wamekwepa majukumu ya kuwahudumia watoto wao na kuwa ni wazi kuwa kuna haja kubwa ya jamii kuendelea kuelimishwa kuhusiana na umuhimu wa kutunza watoto.

Alisema, watoto wana haki ya kulindwa, kuhudumiwa na kupewa mahitaji yote muhimu na kwamba wapo wanaume ambao wameshaanza kutoa matunzo kwa wanawake ambao walikuwa wamewatelekeza na kusisitiza kuwa hatua hiyo inatia moyo lakini aliwataka wanawake kutodanganyika na hatua hiyo kwa kuwa wanaweza kuwakwepa tena.

Updated: 14.04.2018 11:45
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.