Mamia ya Waafrika wanusurika kufa maji wakielekea Ulaya kutafuta maisha

Mamia ya Waafrika wanusurika kufa maji wakielekea Ulaya kutafuta maisha

28 May 2018 Monday 14:19
Mamia ya Waafrika wanusurika kufa maji wakielekea Ulaya kutafuta maisha

Na Mwandishi Wetu

WAAFRIKA kadhaa wamepona kufa maji mara baada ya boti walizokuwa wanasafiri nazo kuokolewa huko nchini Uhispania.

Imeripotiwa kuwa maafisa wa Uhispania wamewaokoa wahamiaji 532 mwishoni mwa wiki iliyopita kutoka kwa zaidi ya boti 15 zilizokuwa zikivuka Bahari ya Mediterenia kwenda Ulaya.

Boti za uokozi za Uhispania zilizifumania boti ndogo nane zilizokuwa zimewabeba watu karibu 250 katika Pwani ya Uhispania jana Jumapili, siku moja baada ya kuwaokoa karibu watu 300 kutoka kwenye boti tisa.

Wahamiaji hao walitokea nchi tofauti za Afrika Kaskazini na Kusini mwa jangwa la Sahara. Tatu kati ya boti zilizokutwa jana zilikuwa katika hali mbaya sana ambapo zilizama muda mfupi tu baada ya watu wote waliokuwamo walipoondolewa.

Hali nzuri ya hewa katika mlango wa Gibraltar, ambayo ndio njia nyembamba zaidi ya Bahari ya Mediterenia inayoitenganisha Uhispania na Morocco, inawafanya wahamiaji wengi kufunga safari hiyo hatari ya kuvuka baharini kwenda Ulaya

Keywords:
Africa
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.