Mbunge wa CCM aitaka serikali kuachana na hadithi

Mbunge wa CCM aitaka serikali kuachana na hadithi

29 May 2018 Tuesday 13:34
Mbunge wa CCM aitaka serikali kuachana na hadithi

Na Mwandishi Wetu

RAPHAEL Chegeni, Mbunge wa Busega (CCM) ameitaka serikali kueleza mikakati ya kuzuia uharibifu wa wanyama pori na kuachana na hadithi.

Alikuwa akiuliza swali la nyongeza kuhusu kuongezeka kwa tatizo la tembo wanaovamia vijiji na kufanya uharibifu wa mali za wananchi.

Aliitaka serikali kueleza mikakati yake kwani wananchi wengi wanapata madhara ikiwemo kuuawa na kuacha hadithi za kuwa watafanya haraka kutatua, au wako mbioni.

Katika  swali lake la msingi Mbunge huyo alisema kuwa kuna migogoro mingi katika hifadhi za taifa na kutaka kujua lini suala hilo litapatiwa ufumbuzi wa kudumu.

Akijbu , Naibu Waziri wa Mali Asili na Utalii, Japhet Hasunga, alisema kuwa serikali kupitia kikosi cha ulinzi wanyama pori (KBU) kimejianga kutatua changamoto mbali mbali kwenye hifadhi zote  kuanzia Julai Mosi Mwaka huu.

Alisema kuwa maeneo mengi yanayopakana na hifadhi za taifa kuna migorogo kutokana na muingiliano wa binadamu na wanyma.

Alisema kuwa migogoro ya mipaka na kuingilia ushoroba wa wanyama kumekuwa kunasababisha madhara makubwa sana.

Aliongeza kuwa ili kupunguza  tatizo hilo,wizara kwa kushirikiana na wadau wameamua kutatua migogoro hiyo kwa kuweka matumizi bora ya ardhi.Alidokeza kuwa watapitia mipaka yote na kuweka vigingi.Pia aliwataka wananchi kuacha kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya shoroba za wanyama .

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.