Ndugai: Baadhi ya Wabunge waliingia mitini kupima Ukimwi

Ndugai: Baadhi ya Wabunge waliingia mitini kupima Ukimwi

29 June 2018 Friday 13:21
Ndugai: Baadhi ya Wabunge waliingia mitini kupima Ukimwi

Na Mwandishi Wetu

BAADHI ya wabunge waliingia hawakushiriki zoezi la kupima virusi vya ukimwi lililokuwa likiongozwa na Waziri Mkuu Kasim Majaliwa huko Dodoma hivi karibuni.

Hayo yamebainishwa na Spika wa Bunge Job Ndugai muda mfupi baada ya Waziri Mkuu  kutoa hoja ya kuahirisha Bunge.

Ndugai aliwashukuru wabunge waliojotokeza kwa wingi katika zoezi hilo akiwemo yeye lakini akasema kuna baadhi waliingia mitini.

Hata hivyo aliwataka wabunge wote kuhamasisha wapiga kura wao kupima ukimwi pindi watakaporudi  majimboni. Aidha Spika alisema kuwa wao kama wabunge tayari wamekwisha fanya kazi ya kuishauri na kuisimamia serikali. Mawaziri walikuwa kikaangoni lakini lengo kubwa lilikuwa ni kuhakikisha kama nchi mambo yetu tunakwenda vizuri” alisema .

Alisema kuwa wabunge wengi  walichangia vizuri na wengine hadi kutoa machozi kwa kuonyesha hisia  na sasa wameondoka bora kuliko walivyokuja wakati kikao kinaanza mwezi wa ApriliAlizishukuru kamati zote za bunge, watendaji na makatibu kwa kufanikisha kikao hicho cha bunge ambacho kimekaa kwa zaidi ya miezi miwili.

Akiahirisha kikao hicho Waziri Mkuu Majaliwa alitoa pole kwa wabunge wenye matatizo ikiwemo Tundu Lissu ambaye alishambuliwa kwa risasi mjini Dodoma mwaka jana.

Bunge limeahirishwa  hadi tarehe 4 mwezi Septemba litakapokutana tena Jijini Dodoma .

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.