Shindano la Tahajia Kufanyika Singida mwezi Septemba

Shindano la 2018 Spelling BEE ni la kwanza kushirikisha watoto wenya mahitaji maluum Afrika Mashariki 

Shindano la Tahajia Kufanyika Singida mwezi Septemba

Shindano la 2018 Spelling BEE ni la kwanza kushirikisha watoto wenya mahitaji maluum Afrika Mashariki 

08 June 2018 Friday 12:03
Shindano la Tahajia Kufanyika Singida mwezi Septemba

Na Mwandishi Wetu, Singida

Zaidi ya wanafunzi 400 wa shule za msingi na sekondari kutoka mkoa wa Singida watajifunza jinsi ya kutelekeza ubora katika tahajia ya maneno kwa njia rahisi na ya ubunifu kufuatia uzinduzi wa shindano la 2018 Spelling BEE uliyofanyika jana, mkoani Singida. 

Shindano hili litafanyika tarehe 29 Septemba mwaka huu katika chuo cha uhasibu Singida.

Madhumuni ya shindano hilo ni kuhamasisha ubora wa mafunzo kwa njia ya ushindani wa tahajia (spelling)  katika lugha ya Kiingereza na Kiswahili, na washariki ni wanafunzi wa darasa la nne hadi kidato cha nne kutoka shule za umma zaidi ya 32 kutoka mkoa wa Singida na inatarajiwa kuwa zaidi ya shule 15 binafsi na za kimataifa watahudhuria shindano hili.

Bi. Upendo Wanguvu meneja mkuu wa Shindano la 2018 Spelling BEE akizungumuza na waandishi wakati wa uzinduzi wa Shindano la 2018 Spelling BEE iloyfanyika leo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida. 

Mkoa wa Singida  kwa ujumla una shule za msingi 551 (za umma 530 na binafsi 22) 164 (za umma 142 na 22 za binafsi) za sekondari ikiwa ni pamoja na shule 4  za wanfunzi wenye mahitaji maluum.

Kitaifa shule za halmashauri za wilaya ya Itigi na Manyoni zinafanya vizuri katika mkoa wa Singida katika mitihani ya darasa la 7 na kidato cha nne.

Ufaulu wa halmashauri ya  Itigi kwa mtihani ya darasa la 7 mwaka wa 2017 ilikuwa nafasi ya 56 kati ya halmshauri 186 nchini, na ufaulu wa halmashauri ya ya Manyoni  katika mitihani ya kidato cha nne ni nafasi 47 kati ya halmashauri 186.  

Pamoja na ufaulu huu mzuri uliojionyesha kwa halmashauri hizi mbili, kiwango cha ufaulu wa shule zote za sekondari kimepanda ila katika shule za msingi za mkoa ufualu ulishuka kwa ujumla na Mkuu wa Mkoa Dk  Rehema Nchimbi ameahidi kushirilkiana na wadau wote na jamii katika kuboresha elimu mkoani Singinda.  Hii ni kutokana na ujio wa  mpango wa ya kuboresha ubora wa elimu Tanzania – EQUIPT ambayo imeanza kutekelezwa rasmi mkoani Singida kuanzia januari 2018.

Shindano la 2018 Spelling BEE ni la kwanza kushirikisha watoto wenya mahitaji maluum Afrika Mashariki  na ambayo itajumuisha shindano la tahajia la  kingereza na Kiswahili kwa wanafunzi viziwi.

Akizungumza katika uzinduzi wa shindano hilo, meneja wa shindano hili, Bi Upendo Wanguvu alisema, "Leo tumeanza safari ya kuchochea ubora wa elimu kwa shindano la tahajia ambalo tumelenga shule za msingi na sekondari nchini Tanzania.

Tunauhakika ya kwamba mashindano yetu yatahamisha ustadi wa wanafunzi kujifudisha maneno, maana ya maneno, jinsi ya kutumia maneno katika sentensi na tahaji ya maneno na hii ni mojawapo ya msingi bora wa elimu.

Safari yetu mwaka huu imeanza mkoani  Singida na tunatarajia ya kwamba shindano hili litajumuisha mikoa yote 31 ndani ya miaka mitatu ijayo. Aidha, uzinduzi wetu leo unafungua rasmi wigo wa kujisajili kwa shule binafsi na za kimataif kwa kutumia tovuti yetu ya www.spellingbee.co.tz ya shindano letu ”

Shindano la Special Needs BEE ni la wanafunzi viziwi ambalo itafinyika kwa lugha ya Kiswahili na kingereza na wanafunzi watafanya tahajia kwa lugha ya ishara. Matuamani ya shindano hili ni kuwa zaidi wa wanafunzi 100 kutoka shule za maitaji maalum mbalimbali Tanzania watahudhuria.

Akizungumza juu ya Shindano la Special Needs BEE Bw. Yasin Mawe, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Tanzania la Viziwi alisema "Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Tanzania na Afrika Mashariki kuwa na shindano la tahajia ambalo limehusisha wanafunzi viziwi.

Ushirikiano kati ya  wanafunzi wenye mahitaji maalum na wanafunzi wengine ni nguzo kuu ya maendeleo na tunafurahia ya kuwa mashindano ya 2018 Spelling BEE imejumuisha swala hili  na itajenga msingi mzuri wa ushirikiano kati ya watu wa mahitajii maalum na wengine.

Shindano hili limeandaliwa na Cece & Daniel Enterpise wakishirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), Taasisi ya Elimu ya Tanzania (TIE), Taasisi ya Africa For Inclusive Communities (AFIC), Shirika la viziwi Tanzania pamoja na ofisi ya rais TAMISEMI na ni mpango wa kipekee wa ushirikiano kati ya mashirika binafsi na mashirika ya umma (Public Private Partnership - PPP).

"Lengo kuu la PPP hii ni kuchochea tabia ya kusoma vitabu miongoni mwa wanafunzi

na tunaamini kuwa ubora wa kujifunza unapatikana pale mwanafunzi anapokuwa anajua maneno, maana yake na jinsi ya kutumia maneno haya katika sentensi. Kwa kawaida maneno yanapatikana katika vitabu na kuhamasisha wanafunzi kujifunza maneno mapya na tahajia ya maneno itasababisha kujenga tabia ya kusoma kati ya wanafunzi "alisema Bi. Upendo.

Alitoa wito kwa makampuni, wadau na wataalamu wa elimu nchini Tanzania kuunga mkono mpango huu wa kipekee wa 2018 Spelling BEE  kwa kushirikiana nao katika shindano hili.

Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) ni wakwanza kuandaa vitabu vya mwogozo wa tahajia ya Kiswahili Tanzania ambavyo vitatumika katika shindano la Kiswahili Spelling BEE na shindano la wanafunzi wenye mahitaji maalum ya Special Needs Kiswahili BEE na vitabu hivyo vimejumuisha mbinu mbalimbali ya kufundisha na kuwaanda wanafunzi kwa ajili ya shindano.

Shindano la 2018 Spelling BEE mwaka huu litatoa zaidi ya zawadi 30 kwa wanafunzi na walimu kwa shule ambazo zitashiriki. Baadhi ya vitengo vya zawadi ni: Wanafunzi Bora wa Tahajia ya Kiswahili, Kingereza na wanafunzi wa mahitaji maalum, Walimu Bora, Mshiriki wa umri mdogo, Wanafunzi bora wa tahajia wa shule za Umma, Wasichana bora wa tahajia na Wanafunzi Bora wa tahajia katika kila darasa na kidato.

Azania Post

Updated: 08.06.2018 12:18
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.