Tanzania: Serikali inaweza kuongeza mshahara kimya kimya-Waziri Mkuu

Tanzania: Serikali inaweza kuongeza mshahara kimya kimya-Waziri Mkuu

07 June 2018 Thursday 11:40
Tanzania: Serikali inaweza kuongeza mshahara kimya kimya-Waziri Mkuu

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imesema kuwa inaogopa kutangaza kupanda kwa mshahara hadharani kwani kufanya hivyo kuna athari zake kwa  jamii ikiwemo kuongezeka kwa bei ya bidhaa mbali mbali.

Hayo yameelezwa bungeni leo katika kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu  ambapo Mbunge wa Viti Maalum Suzan Lyimo (Chadema) alitaka kujua sababu zinazosababisha serikali kutoongeza mshahara wala kupandisha madaraja wafanyakazi wake kwa muda mrefu

Akijibu swali hilo Waziri Mkuu Kasim Majaliwa , alisema kuwa serikali ina utaratibu wake wa kuwapa stahiki wafanyakazi kadiri wanavyopata. Alisema kupitia idara ya Utumishi wameorodhesha watumishi wote na inaendelea kuboresha maeneo fulani. Aliwataka watumishi wa umma kuwa na imani na serikali na kuwa mpango huo haupotezi fedha na hivi sasa imeanza kulipa madeni.

Alidokeza kuwa nyongeza za mwaka hutolewa  kimya kimya na si lazima kutangazwa hadharani kwani kufanya hivyo kuna athari kubwa kwa jamii.

Alisema serikali haitangazi kuongezeka mshahara bali mtumishi mwenyewe ataona mabadiliko kwenye akaunti yake.Alisema kuwa kutangaza ongezeko la mshahara wakati wa siku kuuu ya wafanyakazi kuna madhara kwani bei za bidhaa zinaweza kupanda na kuathiri na watu ambao si wafanyakazi.

Alisema kuwa  serikali ya awamu ya tano imedhamiria kupunguza gharama za bidhaa sokoni kwa lengo la kuwawezesha wananchi kupata mahitaji ya lazima kwa unafuu.

Azania Post

Updated: 07.06.2018 15:46
Keywords:
Tanzania
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.