Tanzania: Waziri Mkuu aagiza magari yote ya serikali yapelekwe yadi 

Tanzania: Waziri Mkuu aagiza magari yote ya serikali yapelekwe yadi 

27 June 2018 Wednesday 16:29
Tanzania: Waziri Mkuu aagiza magari yote ya serikali yapelekwe yadi 

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI  Mkuu Kasim Majaliwa amewaagiza Watendaji wakuu wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa  gari zote za serikali zinakuwa ndani ya yadi ya mhandisi wa eneo husika mara baada ya muda wa kazi kumalizika.

Ametoa agizo hilo mchana huu wakati akizindua vituo 51 vya utabiri wa wa hali ya hewa vinavyojiendesha wenyewe huko wilayani Bahi mkoani Dodoma

Majaliwa alisema kuwa magari yatakayo ruhusiwa mara baada ya muda huo ni yale yenye kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri husika.

Alisema kuwa kuanzia sasa hakuna dereva yeyote wa gari la serikali atakaye ruhusiwa kubaki na chombo hicho nyumbani kwake.

“Dereva kulala na gari ya serikali nyumbani hapana,” alisisitiza Waziri Mkuu Majaliwa.

Aidha Kiongozi huyo wa nchi aliwataka watumishi wote wa umma wanaoishi nje ya wilaya  ya Bahi kuhamia mara moja ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa.

“Ikifika tarehe 30 mwezi  wa Saba nataka watumishi wote wa Bahi ambao wanaishi nje ya kituo cha kazi wawe wamekwisha hamia, , Mkurugenzi simamia hilo” alisema

Majaliwa alimtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Bahi kumpelekea orodha ya watumishi wote ambao watahamia eneo la kazi na wale watakao kataa.

“Haiwezekani mtumishi anafanya kazi Bahi,   halafu anaishi Dodoma , sasa kama anahitajika na Mkurugenzi atawezaje kufika ndani ya muda? Alihoji.

Akielezea kuhusu vituo hivyo alisema kuwa itasaidia sana kutoa taarifa za hali ya hewa kwa uhakika zaidi.Alisema kuwa kwa sasa  uhakika wa taaarifa hizo ni asilimia  87 lakini  vituo hivyo vitaongeza na kufikia 90.

Alitoa rai kwa watalaam wa kilimo na mifug kutumia taarifa zitakazokuwa zinatolewa na kituo hicho kwa manufaa ya jamii.Aliziagiza wizara za Maji na ile ya Kilimo kutenga  fedha kwa ajili ya kuendeshea vituo hivyo ambavyo ni msaada kutoka UNDP.

Alisema kuwa pindi shirika hilo la umoja wa mataifa likiondoka basi wizara hizo zihakikishe kuwa vituo hivyo vinakuwa endelevu.

Majaliwa pia aliwaasa wanachi kujenga tabia ya kupima virusi vya ukimwi na kujua hali zao kama wameathirika au la. Alisema kuwa endapo watabainika kuwa wameathirika watapatiwa dawa za kufubaza virusi hivyo mara moja bila kungoja hadi kuumwa.

Aliwataka wanaume kuongoza katika kampeni hiyo na kuacha tabia ya kuwategemea wenza wao kupata majibu.Alisema kuwa wanaume hao wanategemea kusikia taarifa za wake zao ambao wamepima na wakisikia mambo mazuri hufurahia jambo ambalo siyo kweli kwani  ugonjwa huo unaambukizwa kwa njia mbali mbali.Aliwataka wananchi waliohudhuria sherehe hizo kujitokeza kwa wingi kupima VVU kwenye gari lililokuwa limepaki pembeni.

Awali Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu(Sera, Bunge , Kazi, Vijana , Ajira na watu wenye ulemavu ) Jenista Mhagama alisema  kuwa uzinduzi huo ni baadhi ya jitihada zinazofanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendele katika kuhakikisha menejment ya maafa inamarika nchini.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.