banner68
banner58

Benki ya wanawake yaponea chuchupu, ni baada ya serikali kuamua kuipa nguvu

Benki ya wanawake yaponea chuchupu, ni baada ya serikali kuamua kuipa nguvu

16 May 2018 Wednesday 20:01
Benki ya wanawake yaponea chuchupu, ni baada ya serikali kuamua kuipa nguvu

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imesema kuwa itaongeza mtaji wa benki ya wanawake Tanzania (TWB) ambayo kwa sasa inakabiliwa na matatizo makubwa ya kifedha ili iweze kujiendesha.

Hayo yameelezwa na Naibu waziri wa fedha na Mipango Dk Ashati Kijaji alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Bupe Mwakang’ata (CCM) aliyetaka kujua sababu za benki hiyo kushindwa kutoa mikopo kwa wanawake.

Akijibu Naibu Waziri alisema kuwa kwa sasa benki hiyo ina changamoto nyingi zinazosababisha kushindwa kufanya kazi vizuri.

Alisema kuwa kwa sasa serikali imeona umuhimu wa kuangalia upya sheria ya taasisi za fedha nchini Tanzania.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 9 wa Umoja wa wanawake mwishoni mwa mwaka  jana,Rais Dk John Magufuli alisema kuwa hajaridhishwa  na utendaji wa Benki hiyo hivyo ataipitia upya, kuiangalia vizuri na kuichambua.

Rais Magufuli alisema hajaridhishwa na utendaji wa banki hiyo kwani haijakidhi matakwa ya kuanzishwa kwake ili kusaidia wanawake, lakini kwa bahati mbaya wakopeshwaji wakubwa wa benki hiyo amekuwa si wanawake badala yake wamekuwa wanaume.

Aidha Rais Magufuli alisma benki hiyo haijasambaza matawi katika mikoa mingine nchini, matawi yote ya benki hiyo mengi yapo jijini Dar es Salaam.

“Hili la Benki ya Wanawake Tanzania lazima niwaeleze ukweli, haifanyi vizuri nikiwaficha nitakuwa mnafiki, tangu kuanzishwa kwake na mtaji kupewa bado utendaji wake hauridhishi,” alisema na kuongeza:“Nataka niwaeleze, hata wanaokopa hapo si wanawake na riba ni kubwa kweli kwa wanawake, sasa unakuwa na benki ya wanawake lakini haiwasaidii badala yake inawaumiza wanawake”.

Rais Magufuli alibainisha kwamba kutokana na hali hiyo watapitia upya na kuichambua vizuri ili iweze kukidhi matakwa ya kuanzishwa kwake.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.