Bilionea wa Kifaransa ampiku Bill Gates kifedha

Bilionea wa Kifaransa ampiku Bill Gates kifedha

18 July 2019 Thursday 18:18
Bilionea wa Kifaransa ampiku Bill Gates kifedha

BILIONEA, Bill Gates ameshuka kwa nafasi moja hadi ya tatu katika orodha ya watu wenye ukwasi(fedha) zaidi  kote Duniani.

Kwa takriban miaka saba mfululizo Bill Gates ambaye ni mwanzilishi wa Microsoft na mwenye ukwasi wa dola bilioni 107 sasa ameshushwa hadi nafasi ya tatu na bilionea wa Kifaransa, Bernard Arnault ambaye anashika nafasi ya pili.

Ripoti ya Bloomberg Billionaires sasa inamtaja Arnault ambaye ni mfanyabiashara na mkurugenzi mkuu wa bidhaa za LVMH, kuwa anaukwasi wa dola bilioni 108.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo nafasi ya kwanza  bado inaendelea kushikiliwa na mwanzilishi wa Amazon, Jeff Bezos ambaye ana utajiri wa  dola bilioni 124.

Updated: 18.07.2019 18:26
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.