KCB  kutoa ruzuku milioni 5 kwa wajasiliamari wanawake

KCB  kutoa ruzuku milioni 5 kwa wajasiliamari wanawake

14 June 2019 Friday 09:32
KCB  kutoa ruzuku milioni 5 kwa wajasiliamari wanawake

Na Francis Peter, Dar es Salaam
BENKI ya KCB Tanzania  inatarajia kutoa ruzuku ya milioni 5 kwa kila mwanamke ambaye ni mjasiliamari

Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na  mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo, Christine Manyenye.

Amesema kupitia mpango huo KCB imewawezesha wanawake 256 kwa kuwapa mafunzo ya kuwaongezea wigo wa masoko ili kukuza mitaji na biashara zao.

Manyenye amesema kupitia programu ya 2jiajiri kwa mwaka 2019 itafanyika kwa awamu mbili, awamu ya kwanza ni utoaji mafunzo kwa nadharia katika kurasimisha biashara, usimamizi wa fedha na kuongeza mauzo.

Amesema  katika idadi hiyo(256), wanawake 115  wamepitia mafunzo kwa vitendo.

Bi. Christine amesema japo ruzuku hiyo haina marejesho, Benki ya KCB itaendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo ya wapokeaji ili kuhakikisha wanawake hao wanafikia malengo.

Pamoja na mambo mengini vigezo vya kupewa ruzuku hiyo ni  lazima mpokeaji awe amekamilisha mafunzo ya kinadharia na vitendo katika awamu ya kwanza, awe muendesha akaunti ya 2jiajiri iliyo hai na awe mwenye cheti na leseni halali ya usajili wa biashara.

Updated: 14.06.2019 10:40
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.