Kosa la udanganyifu laiponza kampuni kubwa la magari huko Ujerumani

Magari yake zaidi ya milioni 10 yatumika bila kuwa na progamu mahsusi ya kompyuta

Kosa la udanganyifu laiponza kampuni kubwa la magari huko Ujerumani

Magari yake zaidi ya milioni 10 yatumika bila kuwa na progamu mahsusi ya kompyuta

14 June 2018 Thursday 17:24
Kosa la udanganyifu laiponza kampuni kubwa la magari huko Ujerumani

Na Mwandishi Wetu

MAHAKAMA nchini Ujerumani imeitoza faini mamilioni ya euro kampuni ya kubwa ya magari ijulikanayo kama Volkswagen kwa kukosa uaminifu.

Imeripotiwa kuwa Volkswagen imepigwa faini ya euro bilioni moja, kwa kuruhusu magari milioni 10.7 kwenda barabarani kati ya mwaka 2007 na 2015, yakitumia programu ya komputa isiyoaminika ya kuratibu utoaji wa gesi.

Magari hayo yaliuzwa nchini Marekani, Canada na kwingineko duniani.

Adhabu hiyo iliidhinishwa na mahakama ya mjini Braunschweig ulio karibu na makao makuu ya kampuni hiyo mjini Wolfsburg.

Volkswagen imesema inatumai kuwa kulipa faini hiyo kutasaidia kusafisha haiba yake iliyotiwa doa na makosa yake ya siku za nyuma, na kuzuia mienendo kama hiyo siku za usoni.

Taarifa za uanganyifu katika mfumo wa utoaji wa gesi chafu katika magari ya Volkswagen uligunduliwa na wachunguzi wa kimarekani Septemba 2015.

Ugunduzi huo uliilazimisha kurejesha kiwandani mamilioni ya magari, na kuichafua sifa ya kampuni hiyo.

Volkswagen bado inakabiliwa na kesi nyingine 19 kuhusiana na udanganyifu huo nchini Marekani, Canada, India, Brazil, China na Australia.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.